Vera Sidika azungumzia mipango ya harusi yake

Brown na Vera hawakufanya harusi kubwa ya kanisa.

Muhtasari
  • Vera amefichua kuwa sababu ya yeye kuchukua muda wake ni kutaka kufanya moja ya harusi kubwa Afrika Mashariki

Vera Sidika ni mmoja wa watu mashuhuri nchini Kenya. Vera amekuwa kwenye tasnia ya umaarufu kama mtu mashuhuri kwa zaidi ya miaka kumi.

Kwa sasa Vera ana wafuasi zaidi ya milioni mbili kwenye akaunti yake ya ukurasa wa Instagram.

Vera kwa sasa ameolewa na Brown Mauzo na wamezaa mtoto mmoja pamoja na mwingine yuko njiani anakuja kwani Vera ni mjamzito.

Brown na Vera hawakufanya harusi kubwa ya kanisa.

Vera na Brown walifanya harusi fupi ya kiserikali katika ofisi ya mwanasheria Mkuu ambapo wawili hao walibeba mashahidi wachache tu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Vera amefunguka kuwa mipango inaendelea na hivi karibuni anapanga kufunga ndoa kubwa na Brown Mauzo.

Vera amefichua kuwa sababu ya yeye kuchukua muda wake ni kutaka kufanya moja ya harusi kubwa Afrika Mashariki.

Mwanasosholaiti huyo alifichua haya baada ya mmoja wa mashabiki kumuuliza'

"Bado unairikiria kufanya harusi kanisani?"

Vera alijibu na kusema;

"Ndio kwa mapenzi ya Mungu itakuwa harusi kubwa kuwahi onekana Afrika mashariki."