Mwaka mmoja wa kofi maarufu la Will Smith kwa Chris Rock katika tuzo za Oscar

Tuzo za mwaka 2023 za Oscar zilishuhudia kila aina ya utani uliorejelea kwa kofi la Smith kwa Rock mwaka jana.

Muhtasari

• Mshereheshaji wa tuzo hizo Jimmy Kimmel alizua utani mara kwa mara kuhusu kofi hilo katika kuongoza tuzo za mwaka huu.

Will Smith akimzaba kofi Chris Rock
Will Smith akimzaba kofi Chris Rock
Image: BBC

Ni mwaka mmoja sasa tangu tuzo maarufu katika tasnia ya uigizaji Oscars kufanyika mwaka jana na tukio kubwa la kofi la mwigizaji Will Smith dhidi ya mchekeshaji Chris Rock kuwa gumzo la mitandaoni kwa sku kadhaa.

Katika wasilisho la tuzo hizo za kila mwaka kwa mwaka 2023, kofi hilo maarufu lilivutwa na kuwa kitovu cha gumzo na utani wote ambapo kila mmoja aliyekuwa akizungumza ni lazima angetupa utani wake kwa kofi alilozabwa Rock na Smith.

Jimmy Kimmel, muongozaji wa kila mwaka wa tuzo hizo za Akademia hakuweza kujizuia kuizungumzia kashfa hiyo kwa njia chache za kipekee.

Kulingana na majarida ya kimataifa, Jimmy Kimmel alianza hotuba yake kuwakumbusha watazamaji kwamba kila mtu anataka wawe salama. "Tuna sera kali zilizopo," alisema. "Iwapo mtu yeyote katika ukumbi huu atafanya kitendo cha vurugu wakati wowote wakati wa onyesho, utapewa tuzo ya Oscar ya Mwigizaji Bora na kuruhusiwa kutoa hotuba ndefu ya dakika 19,” Kimmel alizua utani akirejelea tukio la Smith la mwaka jana baada ya kumzaba kofi mchekeshaji Rock.

"Ikiwa jambo lolote lisilotabirika au vurugu litatokea wakati wa sherehe, fanya tu ulichofanya mwaka jana. Hakuna," Jimmy alitania. "Kaeni hapo na msifanye chochote. Labda hata mkumbatie mshambulizi. Na ikiwa yeyote kati yenu atakasirishwa na mzaha na kuamua kutaka kuupuzilia - haitakuwa rahisi." – jarida la E News liliripoti.

Baadaye katika saa ya kwanza, Jimmy alisaidia kutambulisha watangazaji wawili wa kitengo cha Kipengele Bora cha Makala, ambapo "tulikuwa na mzozo huo mdogo mwaka jana."

"Tunatumai wakati huu itamalizika bila shida, au angalau bila utata," Jimmy alitania huku akinukuu maneno kwenye filamu ya Will ya 2005. "Tafadhali weka mikono yako pamoja kisha iweke kwako kwa washindi wa Oscar Riz Ahmed na Questlove."

Takriban saa mbili za onyesho, Jimmy pia alikubali maendeleo ya onyesho. Lakini kuna kitu kilikosekana kutoka kwa tukio la moja kwa moja?

"Vipi nyie mnaendelea? Kila mtu yuko sawa? Mnaning'inia huko?" Aliuliza kutoka jukwaani. "Niliweka chakula chini ya viti vyenu, sijui kama mmegundua. Hatua hii katika aina ya shoo inakufanya ukose lile kofi kidogo, sawa?" alizua utani tena.