Amber Ray na Rapudo wabarikiwa na mtoto msichana kisiri

Amber Ray na mchumba wake Kennedy Rapudo wamebarikiwa na mtoto wao wa kwanza pamoja.

Muhtasari

•Siku ya Jumatatu, Amber Ray alishiriki habari hizo njema kupitia mitandao ya kijamii akimkaribisha mtoto wake wa kike ulimwenguni.

•Wakati huo huo, Rapudo pia aliweka picha za mpenzi huyo wake akiwa hospitalini baada ya kumkaribisha mtoto wao.

Amber Ray na Kennedy Rapudo wamkaribisha mtoto wao wa kike.
Amber Ray na Kennedy Rapudo wamkaribisha mtoto wao wa kike.
Image: HISANI

Mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray na mchumba wake Kennedy Rapudo wamebarikiwa na mtoto wao wa kwanza pamoja.

Siku ya Jumatatu, Amber Ray alishiriki habari hizo njema kupitia mitandao ya kijamii akimkaribisha mtoto wake wa kike ulimwenguni.

"Kuhusu msemo 'unaishi mara moja tu" Ninaanza kujiuliza jinsi hiyo ni kweli! Je, inaweza kuwa kweli kwamba siku moja ni kama miaka elfu na miaka elfu kama siku? Ninaweza kuwa na maswali machache zaidi ambayo hayajajibiwa, lakini kwa sasa...

"Mtu wangu yuko pamoja nami kama malaika wa nyumba yangu na mimi ni mama mpya kabisa! Karibu nyumbani mtoto A...nimekuhisi maisha haya yote na sasa naweza kukuona, kukusikia, na kukugusa...NI MAISHA MPYA KABISA 🙌🏾 Maisha ya maisha mengi," Amber Ray aliandika.

Wakati huo huo, Rapudo pia aliweka picha za mpenzi huyo wake akiwa hospitalini baada ya kumkaribisha mtoto wao.

"Niliangalia jinsi ulivyobadilika kila siku na nilishangazwa na nguvu zako baby love. Sikuweza kufikiria mkazo wa kubeba binadamu mwingine mwilini maana sijawahi kukumbana na hilo.

"Ulinifundisha nguvu ya kweli ni nini kwani ulivumilia kila teke na mabadiliko ili kunipa mtoto. Wewe ni mzuri na ninashukuru kwa zawadi yako. Umethibitisha tena kwamba umeundwa kwa ajili yangu maalum. Hongera baby love @iam_amberay 🍾🥂," Kennedy Rapudo aliandika.

Hospitali ya Nairobi, pia ilishiriki picha ya Amber Ray akiwa katika kituo chao akimpongeza mama huyo mpya.

Hili linawashangaza wengi, kwani Amber Ray bado yuko bize kuchapisha picha kutoka kwa picha yake ya kupendeza ya uzazi akiwa na mchumba wake Kennedy Rapudo