Masalale! Yafichuliwa Zari alitaka kupata mtoto mwingine na Diamond licha ya kutengana

"Zari alitaka mtoto mwingine nami. Alitaka kupata mtu wa kumzalia mtoto," Diamond alifichua.

Muhtasari

•Diamond aliambia mshikaji wake mpya kuwa mpenzi wake wa zamani na mama wa watoto wake, Zari Hassan alitaka mtoto mwingine naye.

•Hivi majuzi, Zari aliwaambia waandishi wa habari kwamba angependa kupata watoto wengine watano na mumewe Shakib.

Zari Hassan ,Diamond Platnumz na watoto wao Tiffah na Nillan.
Image: HISANI

Mwimbaji Diamond Platnumz aliambia mshikaji wake mpya kuwa mpenzi wake wa zamani na mama wa watoto wake, Zari Hassan alitaka mtoto mwingine naye.

Diamond na rapa wa Ghana Fantana wamezama kabisa ndani ya mahaba na aliionyesha kwenye reality show ya Young, Famous, and African.

Zari na Diamond ni wazazi wa watoto wawili, Princess Tiffah na Prince Nillan.

"Zari alitaka mtoto mwingine nami. Alitaka kupata mtu wa kumzalia mtoto," Diamond alifichua kwenye kipindi hicho.

Kwa sasa Zari ameolewa na kijana kutoka Uganda, Shakib Cham ambaye hivi majuzi aliwaambia waandishi wa habari kwamba angependa kupata watoto wengine watano naye.

Mwanasosholaiti huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa lugha ya Kiganda alisema yuko tayari kumpa mume wake watoto na kuongeza kuwa yeye pia yuko tayari kuolewa.

Pia aliwaambia waandishi wa habari kwamba Shakib ndiye mume wake wa kwanza halali ambaye alifunga naye ndoa rasmi.

Aliyekuwa mpenzi wake marehemu Ivan Semwangaalikuwa tu na sherehe ya kutambulishwa kwa wazazi lakini hawakuwahi kufunga ndoa. Wawili hao walizaa wavulana watatu.