Seneta Karen Nyamu awashauri vijana kutobagua kazi

Karen Nyamu aliwahimiza vijana kuchukua kazi bila kujali kama anajua jinsi ya kufanya kazi hiyo au la.

Muhtasari

• Karen Nyamu alipakia picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa kwenye chumba cha kutunzia ndege kinachodhaniwa kuwa alikuwa akifanya ukarabati.

Karen Nyamu awahimiza vijana kuchukua kazi bila kujali wanajua jinsi ya kufanya kazi hizo au la.
Karen Nyamu awahimiza vijana kuchukua kazi bila kujali wanajua jinsi ya kufanya kazi hizo au la.
Image: Instagram

Seneta maalum Karen Nyamu amewahimiza vijana kuchukua kazi bila kujali.

Nyamu ambaye ni seneta maalum wa chama cha UDA alipakia picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa kwenye chumba cha kutunzia ndege kinachodhaniwa kuwa alikuwa akifanya ukarabati.

Nyamu alisema kuwa na hii uchumi ya sasa mtu yeyote hafai kukataa kazi kwani iwapo kazi iko unachukua tu bora wanalipa.

"Tulisema na hii uchumi usikata kazi. Bora kazi iko unachukua tu. Ukiskia wanatafuta mhandisi wa ndege unachukua tu. Usijali kama hujui hiyo kazi utajulia mbele. Bora wanalipa unachukua kazi," Nyamu aliandika kwa mbwembwe.

Mashabiki wake walitoa maoni tofauti tofauti kuhusu picha hiyo aliyopakia kwenye ukurasa wake huku wengine wakimtania.

"Haki hivi ndivyo ninavyoendelea kuwaambia wenzangu... hata ya rubani chukua utajulia kundesha kwa hewa alaar... hii uchumi ni mbaya," megmbuthia aliandika.

"Na wakitaka rubani unajituma unafurusha kitu abiria watajulia mbele kama uko hewani," gichuhigithaiga aliandika.

"Sasa unafungua nini hapo hata hakuna kitu ya kufunguliwa na saizi hiyo ya spana hapo," Deey3540 aliandika.

"Nipige moja nikijifanya nafungua," mc_maspeedy_ aliandika.

"Sio uchumi ni serikali yenyu. Mlidanganya maskini na hivi karibuni Mungu atawakamata," partner_skyfall aliandika.

"Hi Mhesh... Hata mzee tulisema usishughulike kujua uko nambari ngapi bora uko kwa list," assonie33_ aliandika huku akimalizia na emoji ya kicheko.