OMONDI KUOMBA PESA

Eric Omondi aomba msaada wa fedha London kusaidia maskini

Alikusanya 340,000 kuwasaidia Wakenya wachache kupata unga

Muhtasari

•Wakiomba, tunaomba. Nikiwa UK, nilichukua muda kukusanya pesa katika barabara za London ili nije kuwasaidia Wakenya wenzangu maana hali ni mbaya. Niliweza kukusanya Ksh 340,000 ambazo nitatumia kuwanunulia Wakenya wachache unga.

•Omondi alikutana na kiongozi wa chama cha Roots Party Prof. George Wajackoya, kujadili na kutoa suluhu mwafaka za baadhi ya matatizo yanayowakumba vijana nchini Kenya.

Image: Instagram// Eric Omondi

Mkuza maudhui Eric Omondi ameonyesha hisia za huruma aliyonayo kwa Wakenya wanaolala njaa pamoja na wakuza maudhui wenzake ambao hawana vipakatalishi vya kufanyia kazi zao.

Omondi aliposti kanda ya video akiwa Uingereza akiomba msaada wa pesa katika barara za mji huo ambao pia alitaja kuwa kuna baadhi ya Wazungu ambao wanaendeleza ubaguzi wa rangi hasa video hiyo ilipoonesha kudhulumiwa kwake.

Mchekeshaji huyo alieleza kuwa katika safari yake huko London, hakutoka bure maana alikusanya shilingi 340,000 ambazo atatumia kuwanunulia baadhi wa Wakenya unga na pia kuwasaidia wakuza maudhui wachache kununua vipakatalishi.

“Wakiomba tunaomba...While in the UK I took sometime to Raise some money in the Streets of London to come and support fellow Kenyans juu sasa nikubaya. I managed to Raise Ksh 340,000 which I will use to buy Unga for a few Kenyans and Laptops for upcoming Content Creators. (Alafu sasa kuna huyo Mzungu racist🤦‍♂️🤦‍♂️)” Omondi aliposti.

 

Ambayo tafsiri yake ni, Wakiomba, tunaomba. Nikiwa UK, nilichukua muda kukusanya pesa katika barabara za London ili nije kuwasaidia Wakenya wenzangu maana hali ni mbaya. Niliweza kukusanya Ksh 340,000 ambazo nitatumia kuwanunulia Wakenya wachache unga na vipakatalishi kwa waunda maudhui chipukizi.Ila, kuna huyo Mzungu mbaguzi wa rangi.

Haya yanajiri siku chache, wakati ambapo Omondi alikutana na kiongozi wa chama cha Roots Party Prof. George Wajackoya, kujadili na kutoa suluhu mwafaka za baadhi ya matatizo yanayowakumba vijana nchini Kenya.