Marioo aahidi kumnunulia Frida Kajala zawadi ghali ili kuthamini jinsi alivyomzalia mpenzi mrembo

Paula Kajala kwa hasira nyingi aliwasuta watu wanaoingilia maisha yake hasa ya mahusiano.

Muhtasari
  • Hii ni kwa sababu Marioo anataka kumthamini sana Frida Kajala kwa kumpa mpenzi mzuri, ambaye ni mtoto wake Paula Kajala.
Marioo na Paula
Image: INSTAGRAM// MARIOO

Mwimbaji mashuhuri wa Tanzania Omary Ally Mwanga almaarufu Marioo anatazamiwa kumshangaza mama mkwe wake mtarajiwa Frida Kajala kwa njia kubwa.

Msanii huyo kibao cha 'Lonely' leo ameahidi kutumia pesa zake, na kumnunulia gari jipya mwigizaji huyo maarufu wa Bongo movie.

Hii ni kwa sababu Marioo anataka kumthamini sana Frida Kajala kwa kumpa mpenzi mzuri, ambaye ni mtoto wake Paula Kajala.

Mwimbaji huyo alifichua hayo kwenye akaunti yake ya Instagram, na kushiriki video fupi ya mwanzilishi wa sassy Paulah Closet.

Marioo aliongozana zaidi na video hiyo na nukuu iliyojaa sura ya Paula Kajala akisema:

"Kwa uzuri huu lazima ninunue gari kwaajir ya mama mkwe πŸ‘β€οΈβ€πŸ”₯".

Hata hivyo hakuwahi kufichua aina ya gari ambalo atamnunulia.

Hatua ya Marioo kutaka kumthamini mama mkwe wake mtarajiwa Frida Kajala imekuja miezi michache tu baada ya kuanza kuchumbiana na bintiye Paula Kajala.

Pia alisifia urembo wa Paula huku akisema kwamba Mungu alimuumba vyema na hamna mwanamke mrembo zaidi kumshinda.

"Sawa kuna wanawake wengi wazuri ila nyie huyu Mtoto hapana πŸ™ŒHapa mungu kajua namna ya kuifanya kazi yake πŸ™ŒπŸ™ˆπŸ˜₯πŸ˜β€οΈβ€πŸ”₯."

Paula Kajala kwa hasira nyingi aliwasuta watu wanaoingilia maisha yake hasa ya mahusiano.

"Ifike mahala mheshimu maisha ya mtu binafsi, nina haki ya kuwa na mtu nimpendaye kama watoto zenu/ndugu zenu/na nyinyi wenyewe mnavyofanya (Tofauti yetu, nyinyi mnafanya gizani mimi ninawaonyesha)," alisema.

Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20 aliwataka wakosoaji kuangazia familia zao na kutoingia maisha yake.

"Mungu tu anaweza kunihukumu! Nyie waungu watu wa kwenye mitandao muda huu mngeutumia kuabudu makanisani/ msikitini na mngekuwa mmekokoa roho za watu wengi kuliko hichi mnachokifanya. Nimewachoka," alisema.

Paula alidokeza kuwa baadhi ya wakosoaji walitaka kumuona amehuzunika baada ya kuachana na Rayvanny mwaka jana. Aliendelea kubainisha kwamba anamshukuru Mola kwa kumbariki na kumbariki na bavu lake, Marioo.

"Mniache niishi kwa amani mnitoe kwenye midomo yenu hata nikiharikiwa nyie inawahusu nini kwa sababu hakuna ata mmoja anayenisaidia mpaka hapa nilipo. Achaneni na mimi mfocus na maisha yenu. Maisha yangu yatawasumbua na hakuna cha maana mtakachokipata kwa kuniongelea mimi vibaya," alisema.

 

 

 

 

Marioo na Paula
Image: INSTAGRAM// MARIOO