Nimechoka kuwa mtu mzuri kwa miaka mingi-Jovial

"Hawakupendi, wanapenda unachotoa! Wahitaji tu kidogo, hawapatikani kamwe!" Jovial aliandika.

Muhtasari
  • Jovial pia alibainisha kuwa watu hawatakupenda au kukukosoa kwa kusema "hapana" kwa sababu tu wamekuzoea kila wakati kusema "ndiyo."

Mwimbaji Jovial alitumia akaunti yake ya Instagram kueleza kwamba alikuwa amemaliza kujaribu kuwa mtu mzuri kwani ilikuwa imemchosha.

Aidha alieleza kuwa hali hiyo inamchosha haswa msanii kwani huwa wanatoa sana hadi wanakosa cha kutoa.

Jovial pia alibainisha kuwa watu hawatakupenda au kukukosoa kwa kusema "hapana" kwa sababu tu wamekuzoea kila wakati kusema "ndiyo."

"Hawakupendi, wanapenda unachotoa! Wahitaji tu kidogo, hawapatikani kamwe!" Jovial aliandika.

Alihitimisha kuwa kuwa mtu mzuri mara nyingi huhisi kama laana kwa sababu licha ya kuwafurahisha wengine, unaweza kuishia kuteseka.

 

Jovial alionyesha kwamba watu huwa wanatambua na kuthamini wema wako baada tu ya wewe kuondoka, kwani watazungumza tu jinsi ulivyokuwa mzuri wakati huo.

Alionyesha kwamba inaweza kuvunja moyo kutambua kwamba kutambuliwa kwa wema wako kunaweza kuchelewa sana, na huenda ukalazimika kuvumilia mapambano ya kibinafsi njiani.

"Wahitaji tu kidogo hawapatikani,kuwa na roho nzuri ni kama laana unahumia tu kufurahisha watu alafu unakfa maskini wanabaki kusema alikuwa mtu mzuri."

Mwanamziki Jovial aliwachilia wimbo wake mpya hivi majuzi alimyomshirikisha Lexsil.

Wimbo huo uliibua gumzo mitandaoni baada ya muigizaji Bahati kuhusishwa kwenye wmbo huo. Bahati kuhusika kwenye video ya wimbo huo ulitokea baada ya yeye kutangaza kusumbuliwa na msongo wa mawazo.

Wanamitandao wengi walichukulia hatua hiyo ya bahati kuwa kama kutafuta kiki ili kuweza kuongeza umaarufu wa wimbo huo.

Kulingana na Jovial, Kurekodiwa kwa video ya wimbo huo "Don’t Give Up" ulimfanya akumbuke kifo cha baba yake mpendwa aliyeaga kutokana na kuugua ugonjwa wa saratani ya ubongo.

"Kurekodiwa kwa wimbo wa 'dontgiveup' ulikuwa mgumu, tulilia sana. kila mtu alikuwa na hadithi zake za kibinafsi na iliniumiza sana. Nilimpoteza baba yangu kwa saratani ya ubongo, jambo ambalo liliniuma sana, hata hadi leo nikikumbuka natokwa na machozi . Kuna siku mimi hukumbuka baba alishimdwa kumtambua mtu yeyote na hata mimi mtoto wake hakuweza kuongea nilipotaka aongee nami, ” alikumbuka.