AKOTHEE AREJEA NCHINI

Akothee amtania mpenziwe kwenye ndege

Omosh aongee Kiswahili au niite Virginia achukue hii chakula

Muhtasari

•Mama huyo wa miaka 43, awali kabla ya fungate hiyo alieleza kuwa alikuwa na mtihani katika Chuo Kikuu Cha Mount Kenya, ambao alitarajia kuufanya na kufuzu kabla ya ziara yake Ugriki.

wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Akothee na mumewe Denis Shweizer wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwimbaji na mwanamuziki Esther Akoth maarufu Akothee amemtania mpenzi wake  Omosh walipokuwa wakirejea kutoka kwenye likizo ya fungate yao Juni 21.

Wapenzi hao walirejea nchini tangu walipozuru Ugriki mnamo Mei 29 kufurahia mapenzi yao baada ya kuzifunga pingu za maisha.

Mama huyo wa watoto watano, aliposti kenye ukarasa kwenye wake wa Instagram kuwa; “Omosh aonge Kiswahili ama niite Virginia Achukue hii chakula.”

Aliendelea kumsifia mpenziwe Omosh kwa ziara hiyo, akieleza kuwa yupo tayari kufika kaunti ya Nakuru siku ambayo ingefuata.“Landed home safe and sound with my husband, Mister Omosh. Thanks alot Kenya Airways flying honeymooners back home  Your flight attendants are very kind, may they be blessed, good morning tukutane Nakuru.”

Ambayo yangetafsiriwa kuwa; nilitua nyumbani salama salimini na mpenzi wangu bwana Omosh, asante sana shirika la ndege nchini la Kenya Airways, wahudumu wa ndege walikuwa wenye huruma sana, wabarikiwe; habari ya asubuhi tukutane Nakuru.

Mama huyo wa miaka 43, awali kabla ya fungate hiyo alieleza kuwa alikuwa na mtihani katika Chuo Kikuu Cha Mount Kenya, ambao alitarajia kuufanya na kufuzu kabla ya ziara yake Ugriki.