Zuchu ashindwa kumuacha Diamond licha ya kumsaliti kimapenzi, waonyesha mahaba hadharani

Wawili hao walionyesha nyakati za kimapenzi ikiwa ni pamoja na kucheza densi za kimahaba pamoja huku wakiwa wameshikana.

Muhtasari

•Diamond na Zuchu walitumia muda mwingi pamoja wakati wote wa harusi hiyo iliyofanyika Milimani City na hata kutoa zawadi pamoja.

•Zuchu alirekodi video iliyomuonyesha akimbusu bosi wake shavuni huku wakiwa wamekaa pamoja kwenye meza moja.

ZUCHU NA DIAMOND PLATNUMZ
Image: WASAFI/INSTAGRAM

Bosi wa WCB, Diamond Platnumz na msanii wake Zuhura Othman almaarufu Zuchu walikuwa miongoni mwa wageni waliohudhuria harusi ya mmoja wa lebo hiyo, Don Fumbwe siku ya Alhamisi jioni.

Mastaa hao wa bongo walitumia muda mwingi pamoja wakati wote wa harusi hiyo iliyofanyika Milimani City na hata kutoa zawadi kwa wanandoa pamoja.

Wakati wakitoa zawadi hiyo pamoja, wanamuziki hao wawili wanaodaiwa kujihusisha kimapenzi walimpongeza Don Fumbwe na mkewe Juju kwa hatua kubwa waliyopiga na kuwapa ushauri wa namna ya kuishi pamoja.

“Sisi tumekuja kutoa zawadi pamoja. Hatuna kikubwa sana, tuna dua. Tunawaombea. Ni vizuri nimuite Zuhura kwa sababu ni mzuri katika hilo (dua),” Diamond alisema kabla ya kumpasha Zuchu kipaza sauti.

Zuchu aliendelea kuwaombea wanandoa hao waishi pamoja kwa maelewano na kuwa na ndoa/familia nzuri.

Video kadhaa za harusi hiyo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha Diamond na binti huyo wa Khadija Kopa wakifurahia muda mzuri pamoja. Wasanii hao wawili maarufu wa bongo fleva walionyesha nyakati za kimapenzi ikiwa ni pamoja na kucheza densi za kimahaba pamoja huku wakiwa wameshikana.

Zuchu alirekodi video nyingine akimbusu bosi wake shavuni huku wakiwa wamekaa pamoja kwenye meza moja. Wawili hao walionekana kuwa na furaha pamoja huku wakicheka na kukumbatiana kwenye video hiyo.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya Zuchu kumrushia bosi huyo wake maneno makali mitandaoni kufuatia madai kuwa alikuwa akitoka kimapenzi na mwimbaji wa dancehall kutoka Ghana  Francine Koffie  Fantana.

Malkia huyo mzaliwa wa Zanzibar alionekana kujawa na ghadhabu baada ya Diamond Platnumz kuonekana akimbusu Fantana katika sehemu ya pili ya filamu halisia ya Young, Famous na Africa kwenye Netflix.

Baada filamu  hiyo kupeperushwa kwenye Netflix mwezi uliopita, mwimbaji huyo wa kibao  'Sukari' alichapisha picha zake kadhaa kwenye mtandao wa Instagram. Pamoja na picha hizo, aliambatanisha video fupi ya mwanamuziki akiimba maneno ya matusi ambayo huenda tusiweze kuchapisha hapa.

Wengi wa wafuasi wake walionekana kutilia maanani sana video hiyo na hata kuihusisha na matukio ya YFA2. Kwa kutaka kujua iwapo video hiyo na matukio ya filamu hiyo yalihusiana, binamu yake Diamond, Romy Jons alichukua hatua ya kumuuliza binti huyo wa Khadija Kopa ikiwa tayari ameshaitazama.

"Umeangalia msimu mpya wa filamu ya Dai? " Romy Jons alimuuliza Zuchu.

Msanii huyo wa WCB aliyeonekana kukerwa na swali hilo alijibu, "Nimeangalia mwaya mwambie nimesema F++k you."

Zuchu na bosi huyo wake walidaiwa kuwa wapenzi kwa muda mrefu hadi walipothibitisha kuachana Februari mwaka huu.

Huku akitangaza kutengana kwao mapema mwaka huu, Diamond aliweka wazi kwamba yeye na Zuchu sio wapenzi tena. Alibainisha yeye na malkia huyo wamebaki kuwa kaka na dada licha ya awali kuonyesha mahaba  makubwa kati yao.

"Kwa pamoja na Zuhura tunaomba tuwataarifu ya kwamba, kwa sasa sisi ni dada na kaka na si wapenzi kama ilivyokuwa ikidhaniwa ama wengine kujua.. Mnaruhusiwa wachumba na wake ama waume kama tutawaridhia," alisema.

Diamond aliongeza, "Lakini muwe na vibarua vinavyoeleweka  sio mje kutuchuna, maana atuhongi hovyo."