"Kwani unatakanga aje?" Seneta Karen Nyamu amuuliza mpenziwe Samidoh baada ya kumtania

Nyamu na Samidoh wameendelea kuonyesha hadharani uhusiano na muungano wao mzuri.

Muhtasari

•Hivi majuzi, seneta huyo wa kuteuliwa alichapisha picha yake nzuri iliyoonyesha mwili wake sawa na uliotunzwa vizuri.

•Huku akimjibu, Karen Nyamu alionekana kushangaa ni nini hasa kinachomridhisha mwimbaji huyo.

Samidoh na Karen Nyamu
Image: HISANI

Wazazi wenza mashuhuri Karen Nyamu na Samuel Muchoki almaarufu Samidoh wameendelea kuonyesha hadharani uhusiano na muungano wao mzuri.

Hivi majuzi, seneta huyo wa kuteuliwa alichapisha picha yake nzuri iliyoonyesha mwili wake sawa na uliotunzwa vizuri.

“Ambia gym instructor wangu kitu!” Karen Nyamu alisema chini ya picha hiyo ambayo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Baba wa watoto wake wawili, Samidoh ni miongoni mwa wanamitandao waliotoa maoni kwenye chapisho hilo.

Staa huyo wa Mugithi alisema kwa kejeli, "Ananyonya kidole sana."

Huku akimjibu, Karen Nyamu alionekana kushangaa ni nini hasa kinachomridhisha mwimbaji huyo.

“Eeh kai wendaga atia mah,” aliandika kwa Kikuyu.

Maana yake,”Eeh, kwani unatakanga aje kweli.”

Wawili hao wanaaminika kuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na tayari wana watoto wawili pamoja, mvulana na msichana.

Takriban wiki mbili zilizopita, wazazi wenza hao walionekana pamoja wakati walipohudhuria siku ya michezo katika shule ya mtoto wao Sam Muchoki Jr.

Kwenye Instagram, Nyamu alichapisha picha na video za hafla hiyo iliyojumuisha michezo ambayo iliwahusisha wazazi na watoto.

Alifichua kwamba mwanawe aliibuka nambari mbili katika mashindano hayo lakini alikuwa akikataa matokeo.

"Siku ya Michezo katika shule ya mwanangu na nina wasiwasi kidogo kwa sababu alikataa kabisa kuwa nambari mbili na kukataa medali yake ya pili," Nyamu alisema.

Aliongezea, "Hii tabia ya opposition tunakemea.

Katika picha alizochapisha Nyamu, Sam Junior alionekana akishindana na watoto wengine uwanjani. Video nyingine ilionyesha Samidoh akiungana na watoto na wazazi wengine katika mchezo. Wote walionekana kufurahia siku hiyo.

Sam Jr ni mtoto wa Karen Nyamu na Samidoh wa kwanza pamoja. Wawili hao pia wana binti pamoja, Taraya Wairimu, ambaye alizaliwa mwaka jana.

Baada ya tukio hilo, seneta Nyamu alilazimika kueleza kwa nini huwa hamuonyeshi baba wa mtoto wake wa kwanza kama anavyojigamba kuhusu baba watoto wake wawili wa mwisho, Samidoh.

Chini ya lake shabiki mmoja alitaka kujua kwa nini seneta huyo hafanyi sawa na mzazi mwenzake mwingine, DJ Saint.

"Na kwa nini huwa hupost baba mtoto wako wa kwanza?" mtumizi wa Instagram alimuuliza.

Seneta Nyamu kwa utani alijibu, "Kwani watu hupost ex zao."

Mcheza santuri wa Kenya, DJ Saint ndiye baba wa mtoto wa kwanza wa Karen Nyamu. Wawili hao walichumbiana kwa kipindi kabla ya kwenda njia tofauti.