Mama ajitokeza kuwalilia na kuwabembeleza wanaume kujitokeza na kuoa mabinti zake - Video

“Wanaume mko wapi? Kama wewe ni mwanaume pale nje, kuna warembo wazuri. Kina baba tafadhali tuma wavulana wenu watoke nje, wasichana wetu wanawatafuta.."

Muhtasari

• "Mnaona hawa wasichana kwenye Instagram wanapakia picha zao wakiwa peke yao, hilo ni tangazo tosha wanauliza ‘mpenzi wangu uko wapi’?"

Mama alilia wanaume kujitokeza na kuwaona binti zake.
Mama alilia wanaume kujitokeza na kuwaona binti zake.
Image: Instagram

Mama mmoja amewashangaza wengi baada ya kufanya video kwenye mtandao wa TikTok akiwaomba wavulana kujitokeza na kuwaposa mabinti zake.

Katika picha hizo za kuchekesha, mama huyo alieleza kuwa mabinti zake wanazeeka na wanahitaji kutafuta mchumba mzuri hivi karibuni.

Pia aliwasihi akina baba wengine kuwahimiza wana wao kutulia na kumchumbia mmoja wa binti zake wa kupendeza.

“Tangazo la umma kwa kila mtu, kwa niaba ya kila mama wa Kiafrika. Tumechoka, tuko na mabinti warembo, wenye miaka 27, 28… wengine hata wanaelekea miaka 33… wako wapi wanaume wa kuwachumbia? Wako wapi? Mnaona hawa wasichana kwenye Instagram wanapakia picha zao wakiwa peke yao, hilo ni tangazo tosha wanauliza ‘mpenzi wangu uko wapi’? Unawapata wako kwenye maeneo ya hadhara na mpenzi wa kufikirika tu,” alisema.

“Wanaume mko wapi? Kama wewe ni mwanaume pale nje, kuna warembo wazuri. Kina baba tafadhali tuma wavulana wenu watoke nje, wasichana wetu wanawatafuta. Ni muda sasa. Ni muda kwa waname kujitokeza,” aliongeza.

Baadhi ya watazamaji walipata video hiyo ya kufurahisha na wakamsifu mama huyo kwa ucheshi na uaminifu wake. Video hiyo ni mojawapo ya video nyingi za mtandaoni za mtandaoni ambazo zimeibua maoni ya waziwazi.

“Kila mama anawatakia watoto wao mema, watu wanazungumza kwenye TikTok na majibu yao yanasikika moyoni 💞 Hii ni mbaya oo,” alisema kwenye chapisho la video hiyo Instagram.

Hii hapa video ya mama huyo: