Mwanamume achapisha picha za uchi za mjane kwenye kikundi cha WhatsApp cha kanisa

Mfanyibiashara huyo alisemekana kumtongoza mjane huyo baada ya mumewe kufa na kuanza kushiriki mapenzi naye huku akimhonga kwa hela, baadae walikosana na akachapisha picha za uchi zaidi ya 50.

Muhtasari

• Mwathiriwa wa pili, Temi, alisema mshukiwa kwa kawaida alifanya naye ngono kwa mfululizo katika migahawa akiwa amenywa dawa za kulevya.

• Hata hivyo, baada ya kutofautiana, alimtumia zaidi ya picha 50 za uchi ambazo alizipiga kwa siri baada ya kufanya mapenzi hotelini.

Image: GETTY IMAGES

Mfanyabiashara mmoja maarufu anayeishi Lagos nchini Nigeria, amegonga vichwa vya habari baada ya kuchapisha picha za uchi za wanawake wajane ambao amekuwa katika mahusiano nao awali kwenye kikundi cha WhatsApp cha kanisa.

Kwa mujibu wa jarida la Punch Metro, mwanamume huyo alichapisha picha hizo kwenye kundi la WhatsApp la kanisa kisha baadae pia akazituma kwa wanafamilia na ofisi ya marehemu mume wa mmoja wa wajane hao.

"Kufikia wakati nitakapomaliza, kujiua litakuwa chaguo lake pekee," mfanyibiashara huyo alisema.

Mmoja wa wajane hao aliyetambulika kwa jina Kester alithibitisha kuwa wakwe zake na mchungaji walimpigia simu kuonyesha mshikamano naye.

Siku ya Jumanne pekee, mfanyibiashara Kennedy alituma picha hizo za uchi kwa angalau watu 48.

Jarida hilo lilikuwa limeripoti katika kipengele maalum Jumapili kwamba wanawake wawili, Kester na mwingine mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Temi, walikutana na Kennedy kando kwenye vikundi tofauti vya gumzo vya WhatsApp na Facebook kwa watu wasio na wapenzi.

Kester, ambaye alifiwa na mumewe takriban miaka minane iliyopita katika ajali ya gari, alisema mfanyabiashara huyo, baada ya kuzungumza naye, alianza kummiminia zawadi za pesa.

Hata hivyo, baada ya kutofautiana, alimtumia zaidi ya picha 50 za uchi ambazo alizipiga kwa siri baada ya kufanya mapenzi hotelini.

Alisema mshukiwa alidai N100,000 [shilingi elfu 18] kutoka kwake kama sharti la kufuta picha hizo.

Mama huyo wa watoto wawili alibainisha kuwa baada ya kutuma pesa hizo na kuuliza ikiwa picha hizo zimefutwa, alidai nyongeza ya N40,000 [elfu 7] ili kuzifuta kabisa, ambazo alimtumia.

Licha ya malipo hayo, mshukiwa aliendelea kusambaza picha hizo kwenye mtandao wa Facebook.

Kester alisema alijaribu kujiua mara mbili lakini alishindwa, kwani baadhi ya walioziona picha hizo walianza kumhoji.

Mwathiriwa wa pili, Temi, alisema mshukiwa kwa kawaida alifanya naye ngono kwa mfululizo katika migahawa akiwa amenywa dawa za kulevya, na baadaye akampa Nauli 1,000 kama nauli ya usafiri, jarida hilo lilifichua.

Alisema baada ya kugundua kuwa hakuwa makini kuhusu uhusiano huo na alikuwa akimtumia tu, aliacha kuzungumza naye.

Hata hivyo, Kennedy aliripotiwa kumtumia picha zake kadhaa za utupu na kudai pesa zote alizotumia kwenye uhusiano huo.