INJILI ISAMBAE

Nachanganya uimbaji wa injili na komedi - Embarambamba

Hujigaragaza kwenye matope na maji chafu kisa na maana uigizaji

Muhtasari

•“Unaona kama kama hii wimbo yangu ya Nataka Nikuingize, wengi wakisikiza watafikiria ni kuingizwa ile hali ya kulala na mwanaume, ila namaanisha nikuingize ndani ya Yesu. Na pia hii nyingine inayosema Imesimama Imesimama, mtu atafikiria ni kwingine lakini kumbe ni injili imesimama!”

Image: INSTAGRAM// EMBARAMBAMBA

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Kenya Chris Embarambamba amekiri kwamba usanii wake wa kuimba nyimbo za injili anauchanganya na maigizo, ili aweze kuzinasa hisia na fikra za mashabiki wake wanaopenda maigizo.

Katika mahojiano na Radio Jambo, baba huyo wa watoto watano alieleza kuwa yeye ni msanii wa nyimbo za injili kiasili, lakini anapenda pia kuchekesha.

Hii ni gospel, original kabisa lakini ndani yake iko na comedy , yaani ni chekesho. Ndio maana najiita the best gospel comedy from Nyanza Kisii. Mimi ni msanii wa Gospel lakini ndani yake najaza comedy, ” alisimulia Embarambamba.

Msanii huyo mwenye utani mwingi huonekana katika kanda za video yake akiyavalia mavazi ya kina dada na kuanza kunengua viuno kama wanafanyavyo kina dada katika maigizo yake ya usanii.

Embarambamba alitoa mifano ya baadhi ya utani anaotoa katika uimbaji wake, huku akieleza kuwa kufasiriwa visivyo na mashabiki ndio unampa umaarufu zaidi na motisha wa kuendelea na kazi yake ya uimbaji.

Unaona kama kama hii wimbo yangu ya Nataka Nikuingize, wengi wakisikiza watafikiria ni kuingizwa ile hali ya kulala na mwanaume, ila namaanisha nikuingize ndani ya Yesu. Na pia hii nyingine inayosema Imesimama Imesimama, mtu atafikiria ni kwingine lakini kumbe ni injili imesimama! Hiyo ndiyo tunaita comedy ndani ya Gospel,”  Aliendelea.

Mwanaume huyo mwenye utata mwingi huimba kwa kujigaragaza kwenye matope na maji chafu, huku akiwa amevalia mararu akijichupachupa kutoka kwenye mti mmoja hadi mwingine,tukio linalowaacha wengi vinywa wazi.