"Alikuwa na upumbavu!" DJ Bonez afunguka jinsi ex wa mkewe Kamene Goro alivyomsumbua

Deejay Bonez alihoji tabia ya mpenzi huyo wa zamani wa mke wake na kusema kwamba alikuwa akitenda kijinga.

Muhtasari

•Wanandoa hao walifichua kuwa mpenzi mmoja wa zamani wa Kamene alipata ugumu wa kuendelea na maisha yake baada ya kutengana na akawa anawafuatilia kuwasumbua.

•“Alikuja akapiga makofi akasema hongera nimeshinda. Niliaita mabouncer wamtoe akatupwa kwa beach. Huyo msee alisumbua,” Bonez alisimulia.

Deejay Bonez na mke wake Kamene Goro
Image: INSTAGRAM// KAMENE GORO

Mcheza santuri mashuhuri David Kamau almaarufu Dejaay Bonez  na mkewe Kamene Goro wamefunguka kuhusu matukio ya kushangaza na mmoja wa wapenzi wa zamani wa mwanahabari huyo.

Wakati wakishiriki hadithi hiyo katika moja ya vipindi vya Kamene and Obinna Podcast, wanandoa hao walifichua kuwa mpenzi mmoja wa zamani wa Kamene alipata ugumu wa kuendelea na maisha yake baada ya kutengana na akawa anawafuatilia nyumbani na hata katika maeneo ya burudani ili kuwasumbua.

Katika tukio moja ambalo walisimulia, wanandoa hao walifichua kuwa mwanamume huyo ambaye hawakutambulisha alikutana nao nyumbani kwa mwanahabari huyo usiku mmoja baada ya kutoka kuburudisha na akaanza kugonga kengele ili wafungue.

“Kuna siku alikuja akalalia kengele ya mlango. Alikuwa anaongea kizungu mingi kwa mlango. Nikamfungulia nikamuuliza kaka ni nini?,” Bonez alisimulia.

Kamene Goro aliendelea kusimulia, “Bonez alianza kuvaa mshipi na viatu nikajua hii ndio ile siku. Tulikuwa tumetoka gig tunachill tu kwa nyumba. Ilikuwa wakati wa Covid. Ilikuwa mwendo wa saa nne usiku. Nilikuwa nimeingia kuoga alafu nikaenda kwa shimo la mlango nikaona ikiwa imezibwa.

Mtangazaji huyo wa zamani wa redio alieleza kuwa tayari alikuwa amemjulisha mumewe kuhusu mpenzi wake wa zamani ambaye alikuwa akimfuata kila mara.

Deejay Bonez alihoji tabia ya mpenzi huyo wa zamani wa mke wake na kusema kwamba alikuwa akitenda kijinga.

“Huyo msee alikuja kuona hatufungui. Akaanza kupiga kengele. Ni upumbavu alikuwa nao,” Bonez alisema.

Kamene alifichua kuwa walijaribu kutafuta usaidizi kutoka kwa walinzi ambao kwa bahati mbaya hawakuweza kutatua mzozo, hali iliyowafanya kuwaita maafisa wa polisi.

“Walinzi walishindwa kutuliza hali. Ikabidi polisi wamepigiwa. Ilibidi beki iingie wakapanda juu wakamtoa,” Kamene alisimulia.

Mtangazaji huyo aliongeza, “Alikuwa anasema amekuja kwa bibi yake. Makarao walikuwa wanamuulizia bibi yako akose kukufungulia aje kama nyumba yako?. Akasema sio kwake ni kwa bibi yake. Akaambiwa huko sio kwake atoke.”

Wanandoa hao pia walishiriki kisa kingine kilichotokea mjini Mombasa ambapo mpenzi wa zamani wa Kamene aliingia katika kilabu ambako Deejay Bonez alikuwa akitumbuiza.

“Tukiwa Mombasa alikuja kwa kundi kubwa la watu akanigusa nikageuka nikashangaa. Ilikuwa kama mwaka mmoja tangu kuachana (Nilikuwa nimekaa na Bonez kama mwaka mmoja na zaidi).. Alisema anataka kwenda kumsalimia mpenzi wangu. Nikasema kwa hatari yako. Akaenda kwa kibanda hapo mbele yake,” Kamene alisimulia.

Bonez alifichua kuwa baada ya kusimama mbele yake, ex wa Kamene alimpigia makofi akimpongeza kwa kushinda mwanamke ambaye ‘walikuwa wakimpigania.’

“Alikuja akapiga makofi akasema hongera nimeshinda. Uzuri Mombasa najulikana na mabouncer. Niliaita mabouncer wamtoe akapelekwa kwa beach. Huyo msee alisumbua,” alisimulia Bonez.

Mcheza santuri huyo hata hivyo aliweka wazi kuwa hawezi kamwe kupigana na mwanaume mwingine kwa sababu ya mwanamke.

“Siwezi mimi sipagi. Siwezi kupigania mwanamke. Kusema ukweli mimi hujiheshimu. Wacha mwanamke aseme mwenyewe aamue anataka nini,” alisema.

Alisema kuwa wakati pekee anaoweza kumtetea mwanamke wake ni pale anaponyanyaswa au kunyang'anywa kitu.

Kamene hata hivyo alionekana kutopenda hisia za mumewe na hata akaomba mazungumzo hayo yafungwe.