"Ninamuonea huruma!" Vera Sidika amfariji ex wake Otile Brown baada ya kupoteza mtoto

"Ni kweli ninamuonea huruma. Rambirambi za dhati kwake,” Vera alisema.

Muhtasari

•Otile Brown alitangaza kwamba yeye na mpenzi wake walipoteza ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza akiwa tumboni bado.

•Vera Sidika alifichua kuwa anasikia vibaya kuhusu hilo na kutuma ujumbe wa rambirambi kwa mwimbaji Otile Brown.

Vera Sidika na Otile Brown wakati wa mahusiano yao
Image: HISANI

Mwanasosholaiti maarufu wa Kenya Vera Sidika amekiri kuwa anamuonea huruma mpenzi wake wa zamani Otile Brown baada ya kumpoteza mtoto wake kabla ya kuzaliwa.

Hivi majuzi, Otile Brown ambaye alichumbiana na mama huyo wa watoto wawili kwa muda mfupi miaka michache iliyopita alitangaza kwamba yeye na mpenzi wake walipoteza ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza akiwa tumboni bado.

Wakati akiwashirikisha wafuasi wake wa Instagram katika kipindi cha Maswali na Majibu siku ya Jumanne, shabiki mmoja alimuuliza Vera Sidika anahisi vipi kuhusu mwimbaji  huyo wa kibao ‘Baby Love’ kumpoteza mtoto wake.

"Otile Brown alisema kwamba amepoteza mtoto hivi majuzi. Najua hilo lazima lilikuwa gumu. Unamuonea huruma?” Mtumiaji wa Instagram alimuuliza Vera Sidika.

Katika jibu lake, mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 33 alifichua kuwa anasikia vibayaa kuhusu hilo na kutuma ujumbe wa rambirambi kwa mwimbaji Otile Brown.

"Ni kweli (ninamuonea huruma). Rambirambi za dhati kwake,” Vera alijibu.

Aliambatanisha ujumbe wake na emoji za kihisia zilizoonyesha jinsi alivyojawa na huruma kufuatia tukio hilo.

Vera Sidika na mwimbaji huyo mzaliwa wa Pwani walichumbiana kwa miezi kadhaa mwaka wa 2018 kabla ya kutengana kwa njia ya kutatanisha. Katika siku za nyuma, Otile Brown aliwahi kudai kuwa walipokuwa wakichumbiana, mwanasosholaiti huyo alipata ujauzito wake lakini baadaye akautoa, madai ambayo Vera amekana mara nyingi.

Siku chache zilizopita, Otile Brown alidokeza hajakuwa akiendelea vizuri tangu alipompoteza mtoto wake ambaye bado hakuwa amejazaliwa.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 30 alifichua kwamba yeye na mpenzi wake walitarajia mtoto wa kiume, ingawa hata hivyo mtoto huyo hakufanikiwa kuishi.

"Alikuwa mvulana. Dah.. Yote ni sawa. Angekuwa besti wangu,” Otile Brown aliandika kwenye Instagram.

Brown alifunguka kuhusu jinsi yule ambaye angekuwa mzazi mwenzake alihusisha kifo cha mtoto wao na hisia mbaya kwenye mitandao ya kijamii baada ya yeye kufichua kuwa alikuwa anatarajia mtoto wake wa kwanza mapema mwezi uliopita, hatua ambayo sasa anajutia.

“Mwanzoni nilichukia mitandao ya kijamii kwa sababu alinichukia na kunifanya niamini kuwa hiyo ni hisia mbaya kwenye mitandao ya kijamii na ni kama ninaamini kwa sababu kwa mtu ambaye hajawahi kutangaza maisha yake kwenye mitandao ya kijamii, kwa bahati mbaya niliamua kuchapisha kuhusu hilo huku moyo wangu ukiniambia nisifanye hivyo, ilinifanya nijihisi kuwa na hatia,” alisema.

Aliongeza, "Lakini tena nilisema siwezi kuipa misismko hii ya chini nguvu nyingi. Huenda ni kosa letu, mpango wa Mungu au sababu za kawaida. Huwezi kubishana nami, haki ya Mungu.”

Mtunzi huyo wa kibao cha ‘Nabayet’ alikiri kwamba kupoteza ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza kulimbadilisha sana.

“Nimekuwa nikihisi huzuni. Nimekuwa nje ya nchi nikiharibu kadi yangu ya malipo, nikijiadhibu. Huwa ninaomboleza tofauti,” alisema.

Mwanamuziki huyo alitangaza kifo cha mtoto wake ambaye bado hakuwa amezaliwa mapema mwezi huu.

Katika taarifa yake, alifichua kwamba yule ambaye angekuwa mtoto wake wa kwanza hakufanikiwa kuishi.

"Mtoto wetu hakufanikiwa.. Nadhani sio mwaka wangu pendwa tena," Otile Brown alisema kwenye mtandao wa Instagram.

Aliongeza, "Yote ni nzuri. Mungu unajua sijawahi kukuuliza wala kukuhoji.. ninachofanya ni kutabasamu na kuwa sawa.