Vera Sidika awacheka wapenzi wa zamani baada ya kurejea mitandaoni kwa picha ya kutongoza

Vera hatimaye ametangaza kurejea kwake katika maisha ya uanasosholaiti baada ya mapumziko ya zaidi ya miaka miwili.

Muhtasari

•Vera alichapisha picha yake ya kuvutia iliyomuonyesa akiwa ndani ya beseni ya kuogea huku akiwa na mavazi mepesi tu yaliyoficha sehemu zake za siri na maziwa yake.

•“Siendi popote. Subirini tu muone,” Vera alijibu baada ya kuulizwa ikiwa amerejea kikamilifu kwenye maisha yake la zamani.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Baada ya kupotea kuchukua mapumziko ya zaidi ya miaka miwili ili kuangazia malezi, Vera Sidika hatimaye ametangaza kurejea kwake katika maisha ya uanasosholaiti kwenye mitandao ya kijamii na chapisho la kusisimua la mwili wake wa kuvutia.

Siku ya Jumatatu, mama huyo wa watoto wawili alichapisha picha yake ya kuvutia iliyomuonyesa akiwa ndani ya beseni ya kuogea huku akiwa na mavazi mepesi tu yaliyoficha sehemu zake za siri na maziwa yake.

"Mimi ndiye kielelezo cha kutongoza. Ninaongeza joto, ninavunja sheria zote na kukumbatia urembo wangu bila msamaha,” aliandika chini ya picha aliyoichapisha kwenye mtandao wa Instagram.

Chapisho hilo lilichukuliwa kuwa tangazo la kurejea kwake katika maisha ya uanasosholaiti baada ya kujifungua watoto wawili katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Baada ya chapisho hilo, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 33 aliwashirikisha wafuasi wake wa Instagram katika kipindi cha Maswali na Majibu ambapo alithibitisha kuwa kweli amerejea kwenye maisha yake ya zamani ya uanamitindo, urembo na usafiri.

“Siendi popote. Subirini tu muone,” Vera alijibu baada ya kuulizwa ikiwa amerejea kikamilifu kwenye maisha yake la zamani.

Shabiki mwingine alidokeza kwamba wapenzi wa zamani wa mwanasosholaiti huyo lazima walichochewa kumtafuta tena baada ya kuona picha ya kutongoza aliyokuwa amechapisha.

"Wapenzi wako wa zamani wote baada ya kuona picha hiyo wanaandika na kufuta," mtumiaji wa Instagram alimwambia.

Alijibu kwa emoji za kucheka kuonyesha hisia zake kuhusu hisia za wapenzi wake wa zamani kwa chapisho lake.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Vera alidokeza mipango ya kurejea katika maisha ya uanasoshalaiti na kusafiri dunia baada ya kujifungua.

Akizungumza kwenye ukurasa wake wa Instagram mwezi Januari, mama huyo wa binti mmoja alidokeza kwamba anapanga kuboresha mwili wake na kusafiri kote duniani tena baada ya kukamilisha hatua ya ujauzito.

Aidha, alionyesha fahari kubwa kwa maendeleo yake ya sasa na mafanikio katika kujenga familia.

"Miaka miwili iliyopita nimekuwa nikizingatia kujenga familia na ninafurahi kwamba hatimaye nilitulia na kuifanya," alisema.

Mke huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo alisifu janga la COVID 19 lililokumba dunia takriban miaka 3 kwa mafanikio yake katika kuanzisha familia huku akieleza kwamba lilimsaidia kutulia na kupata mchumba.

"Maisha yangu yamesawazishwa kikamilifu sasa. Asante Mungu. Kwa hivyo tunarudi kufanya makubwa. Jiandaeni wapenzi, inakaribia kuwa noma," alisema.

Mama huyo wa watoto wawili ni mmoja wa wahusika katika filamu ya uhalisia ya Real Househelps of Nairobi kinachopeperushwa kwenye Showmax. Kipindi hicho kinawashirikisha baadhi ya wanawake mashuhuri nchini Kenya.