Pasta akataa kubariki harusi ya bintiye kwa kugundua Bw. harusi hana Visa ya Kanada (video)

Kwa maoni yake, mwanamume huyo alikuwa akijaribu tu kutumia ndoa ili kupata uraia wa Kanada, na hilo halikumfurahisha akiwa mtu wa Mungu na baba ya bibi-arusi.

Muhtasari

• Matukio hayo yalinaswa katika video iliyotumwa kwenye TikTok na imekuwa ikisambaa kwa kasi, huku watu wengi wakielezea maoni tofauti juu yake.

mchungaji akataa kufungisha harusi kisa bwana harusi hana visa ya Kanada
HARUSI mchungaji akataa kufungisha harusi kisa bwana harusi hana visa ya Kanada
Image: Screengrab

Video moja katika mtandao wa TikTok imewaacha wengi katika mshangao mkubwa baada ya mchungaji wa kanisa moja aliyekuwa amesimamia hafla ya kufanya harusi kukataa kuibariki harusi hiyo alipogundua kwamba Bwana Harusi hakuwa na nyaraka za kuhalalisha kukaa kwake Kanada.

Wageni walioalikwa kwenye harusi hiyo waliachwa na mshangao mkubwa huku mchungaji kiongozi akipandwa na hasira, na kutoka nje ya ukumbi aliotakiwa kubariki harusi kati ya bintiye na kijana mmoja.

Matukio hayo yalinaswa katika video iliyotumwa kwenye TikTok na imekuwa ikisambaa kwa kasi, huku watu wengi wakielezea maoni tofauti juu yake.

Katika video hiyo, bwana harusi alionekana akiwa amesimama mbele ya njia huku wakiwa na wapambe wa upande mmoja huku bibi harusi na wapambe wake nao wakiwa wamesimama upande wa pili, tayari kupokea baraka za mtumishi wa Mungu aliyetokea kuwa baba wa bibi harusi.

Hata hivyo, kwa mshangao wa kila mtu, mchungaji alianza kumhoji kijana huyo kwa ukali mbele ya umati mkubwa wa watu waliohudhuria, ikiwa ana hati ya kisheria ya kumruhusu kukaa Canada, ambapo bwana harusi alijibu hana.

Bila kuridhika na jibu la bwana harusi, mchungaji alishuka kutoka kwenye jukwaa, akambusu bibi arusi kwenye shavu na kusema kwamba hatabariki ndoa.

Kisha akaanza kutoka nje ya ukumbi huku akiguna. Alisimama ili kueleza kutaniko kwamba bwana harusi aliingia Kanada isivyo halali na hangesimamia jambo lisilo halali.

Kwa maoni yake, mwanamume huyo alikuwa akijaribu tu kutumia ndoa ili kupata uraia wa Kanada, na hilo halikumfurahisha akiwa mtu wa Mungu na baba ya bibi-arusi.

“Hana karatasi; Sitakaa hapa na kumsukuma binti yangu …..,” mchungaji asiye na furaha alisema katika video hiyo ya sekunde 48, iliyoandikwa kwa swali, “Ni nini kimetokea sasa hivi?”

Hii hapa video;