Seneta Karen Nyamu awatishia vijana waliojaribu kumtongoza kwa wimbo mchafu

"Hawa nikiwapata ni ma nyahunyu tu," Seneta Karen Nyamu alisema.

Muhtasari

•Nyamu alishiriki video fupi ya vijana hao wakiimba huku wakiinua mabango yaliyoandikwa jina lake na kuambatanishwa na ishara za mapenzi.

•Kufuatia wimbo huo, seneta Karen Nyamu alitoa jibu la utani ambapo alitishia kulipiga kundi hilo la vijana atakapokutana nao.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Seneta mashuhuri wa kuteuliwa Karen Nyamu amevunja kimya baada ya kundi la vijana kutunga wimbo chafu wakimsifu.

Katika ukurasa wake wa Facebook, mama huyo wa watoto watatu alishiriki video fupi ya vijana hao wakiimba huku wakiinua mabango yaliyoandikwa jina lake na kuambatanishwa na ishara za mapenzi.

Wacheza densi waliosimama nyuma ya waimbaji wakuu kwenye video hiyo pia walishikilia picha kubwa ya seneta huyo wa UDA.

“Nani kadogo kazuri (Nyamu)

Kamami kapretty kasupu(Nyamu)

Kanafanya mayouth hatulali (Nyamu)

Nyamu, Nyamu, Nyamu can you be my boo?

Nyamu, Nyamu can you be my boo??

Nyamu can I touch your b**bs?

…...........................

Mahaga za Nyamu, tunazipenda,

Majegi za Nyamu, tunazisherehekea

…..,” vijana hao walisikika wakiimba kwa sehemu kwenye klipu ya video iliyoshirikiwa na seneta huyo.

Kufuatia wimbo huo, seneta Karen Nyamu alitoa jibu la utani ambapo alitishia kulipiga kundi hilo la vijana atakapokutana nao.

"Hawa nikiwapata ni ma nyahunyo tu," alisema.

Nyamu ni miongoni mwa wanasiasa vijana wa Kenya ambao wanajulikana kuwa na sauti nyingi na maingiliano kwenye mitandao ya kijamii. Anajulikana kwa majibu yake ya kejeli na ya ujasiri hasa anaposhambuliwa na wakosoaji.

Yeye pia ni mmoja wa watu mashuhuri wanaozungumziwa sana nchini Kenya haswa kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na mwimbaji wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.

Wiki iliyopita, seneta huyo alilazimika kujibu baada ya imani yake kutiliwa shaka kutokana na chaguo lake la uhusiano.

Mama huyo wa watoto watatu alikuwa amechapisha picha yake kwenye mtandao wa Instagram na chini yake akafichua jinsi Yesu amekuwa naye katika safari yake ya mafanikio.

"Yesu anatembea naye, hiyo ndiyo nguvu yake kuu," Seneta Nyamu aliandika chini ya picha yake akiwa amevalia sare za skauti.

Katika sehemu ya maoni, shabiki mmoja alimshutumu kuwa mharibifu wa ndoa na kusema kwamba Mungu hawapendi watu kama hao.

“Mungu hapendi mtu anaharibu familia ya wenyewe,” dorcasgift6 alimwambia.

Karen Nyamu ambaye alionekana kutopendezwa na maoni ya mtumiaji huyo wa Instagram alijibu, “Nani alisema utaacha kutenda dhambi unapotembea na Yesu. Na tangu lini ndoa ya wake wengi ikawa dhambi.”

Seneta huyo wa UDA mara nyingi amekuwa akishutumiwa kwa kuharibu ndoa ya mwimbaji wa Mugithi  Samuel Muchoki almaarufu Samidoh ambaye ana watoto wawili naye.

Katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita, wawili hao wanaoaminika kuwa wapenzi wameonekana pamoja sana huku mke wa Samidoh wa miaka mingi, Edday Nderitu akiendelea kufurahia wakati mzuri na familia yake nchini Marekani.