Kamene Goro afunguka alivyokutana na mumewe DJ Bonez

Kamene alisema amemfahamu Bonez tangu 2015

Muhtasari

•Kamene alifichua kwamba alikutana na mcheza santuri huyo wakati wa ziara ya Pwani, na kwao, haikuwa mapenzi mwanzoni.

•Bonez alisema muda huo wote alikuwa na namba ya Kamene kwani walikuwa kwenye kundi fulani pamoja.

Deejay Bonez na mke wake Kamene Goro
Image: INSTAGRAM// KAMENE GORO

Mwanahabari Kamene Goro amefichua jinsi alivyokutana na mume wake DJ Bonez.

Wapenzi hao waliwashangaza wengi baada ya picha za harusi yao kuibuka kwenye mitandao ya kijamii mapema mwaka huu.

Katika mahojiano na Oga Obinna, Kamene alifichua kwamba alikutana na mcheza santuri huyo wakati wa ziara ya Pwani, na kwao, haikuwa mapenzi mwanzoni.

“Tulikutana Mombasa, Hatukupendana mwanzoni. Wakati huo rafiki wa Bonez alikuwa na sherehe ya siku ya kuzaliwa, ana klabu. Baadaye nilirudi katika klabu hiyo na mtangazaji mwenzangu wa zamani. Bonez aliwahi kusema mimi ni mzinzi. Nilikuwa mdogo wakati huo." alisema.

Kamene alisema amemfahamu Bonez tangu 2015

"Alinichukia, hatukuwahi kuongea. Mnamo 2020 Desemba nilikuwa na rafiki yangu. Tulitua na tukapelekwa Serena Hotel. Tukaamua kukodisha jahazi, na tuliambiwa tunaweza kupata DJ ndani, kwa hivyo tukakodisha nafasi ya jahazi hilo.

Tulikuwa wawili tu. Sherehe ilianza. Muda si muda nikamuona DJ Bonez, tukazungumza na nikarudi kuongea na marafiki zangu."

Rafiki yangu alikuwa amechukua power bank yangu, yeye (DJ Bonez) alipiga simu na kabla hajasema chochote alichotaka, nilimuelekeza kwa mtu mwingine (Terry). Nilidhani anataka power bank," alisema

Baada ya hapo, alikuwa akija kila siku hotelini na tulikuwa tukijivinjari."

Bonez alisema muda huo wote alikuwa na namba ya Kamene kwani walikuwa kwenye kundi fulani pamoja.