Pasta, mkewe, binti watembea uchi hadharani kuigiza kama Adamu na Hawa [Video]

Baadhi ya Waganda kwenye Twitter wametoa wito wa kukamatwa kwa mtu wa Mungu aliyeripotiwa na mkewe kwa kumdhalilisha binti yao mdogo asiye na hatia.

Muhtasari

• Watu katika jamii walionekana wakikusanyika kumdhihaki pasta, mkewe na binti yao lakini hiyo haikutosha kuwafanya kutengua uamuzi wao.

Mamia ya watu wjitokeza kupigwa picha za uchi
UCHI Mamia ya watu wjitokeza kupigwa picha za uchi
Image: BBC NEWS

Video inayoonyesha mwanamume anayeaminika kuwa mchungaji mmoja kutoka Uganda, mkewe na binti yao wakitembea uchi kabisa hadharani kwa madai ya kufuata nyayo za Adam na Hawa katika mwanzo wa dunia kama inavyosimuliwa kwenye Biblia imeibuka mtandaoni na kuzua hisia nyingi.

Mtumiaji wa Twitter aliyetambulika kama @EricJimmyLevi alishiriki video hiyo ya wazi kwenye ukurasa wake mnamo Jumatatu, ambayo imewaacha watumiaji wa mtandao huo wakijibu kwa maoni ya kufurahisha huku wengine wakihoji hali ya afya ya akili ya familia.

Video hiyo ambayo imesambaa mitandaoni, inaonyesha baadhi ya watu katika jamii walionekana wakikusanyika kumdhihaki pasta, mkewe na binti yao lakini hiyo haikutosha kuwafanya kutengua uamuzi wao.

Baadhi ya Waganda kwenye Twitter wametoa wito wa kukamatwa kwa mtu wa Mungu aliyeripotiwa na mkewe kwa kumdhalilisha binti yao mdogo asiye na hatia.

"Mtoto asiye na hatia, mshike mchungaji na mke sasa!" @withAlvin aliandika.

Mtumiaji mwingine alisema kwamba mtu huyo wa Mungu aliyetajwa lazima alielewa vibaya Biblia Takatifu, hivyo akaweza kushawishi familia yake kuanza misheni hii ambayo inawafanya wadhihakiwe daima.

“Hata Yesu mwenyewe aliwahi kuvaa nguo. Alikuwa na vazi! Kati ni Biblia gani ambayo mchungaji huyo anasoma kwa hakika,” mtumiaji huyo wa Twitter aliandika.

Wakati huo huo, mtumiaji mwingine mmoja wa Twitter ana maoni tofauti na yale ya watumiaji wengine. Hakuona kosa lolote kwa yale ambayo kasisi na familia yake wamefanya.

"Lakini mtu huyu alikuwa sahihi ikiwa sababu ya kufanya hivi ilikuwa ya kweli, wakati mwingine lazima ufanye kisichowezekana ili ulimwengu ubadilike," @starworldwonder aliandika.

Hadithi kadhaa za wachungaji kuwachambua familia zao na washiriki wa kanisa ili kushiriki katika shughuli zinazowadhuru na wakati mwingine kuua zimerekodiwa.

Hivi sasa, nchini Kenya, si chini ya miili 403 ya waumini wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie.

Mtu wa Mungu ameshutumiwa kwa kuendesha ibada na kuwapotosha wafuasi wake isipokuwa wanafamilia wake kuanza mfungo wa siku 40 ili kufa na kukutana na Yesu kwa sababu dunia ilikuwa inaelekea mwisho.