Mwanaume aliyefunga ndoa 3 kwa siku moja anasema lengo ni wanawake 10

Bwana Yengayenga alisema anaishi na wanawake wote ndani ya chumba kimoja lakini anakaa na kila mmoja kwenye kitanda chake siku mbili kwa wiki.

Muhtasari

• Kwa sasa, anaendesha zamu kati ya Fatuma Rafaeli, Asha Pius na Mariam John, na hutumia siku mbili na kila mmoja wao katika wiki.

• Kulingana naye, anahakikisha kwamba anawapa wake wote watatu umakini wa kutosha ili kuepusha mivutano miongoni mwao.

Mwanamume aoa wake 3 ndani ya siku moja.
Mwanamume aoa wake 3 ndani ya siku moja.
Image: Millard Ayo TV

Mwanaume mmoja mwenye mitala ambaye alioa wanawake watatu siku moja katika sherehe moja amesema kuwa kuna wanawake wengi wanaosubiri kwa hamu kuolewa, hivyo ni lazima wanaume watumie fursa hiyo kunyakua zaidi.

Athuman Yengayenga, Muislamu kutoka Shanwe, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi nchini Tanzania alifichua katika mahojiano kwenye YouTube channel ya Millard Ayo ingawa ana wake watatu sasa, lengo lake ni kugonga angalau kumi.

“Hawa watatu hawatoshi. Kuna wanawake wengi huko nje wanasubiri kuolewa. Hawatakiwi kutafutwa kwani ni suala la kuzungumza nao na kuwasilisha wazo lako. Nawasihi wanaume wasilale kwenye fursa hii bali washambulie wakiwa tayari,” alisema kwenye mahojiano hayo.

Yengayenga aliongeza kuwa pamoja na kwamba yuko tayari kuwa na wake zaidi, lakini atalazimika kupata ridhaa ya watatu alionao ili aendelee kwa sababu amani na utangamano wa nyumbani ni muhimu kwake.

"Kama wanasema ndiyo, basi nitaendelea. Wakisema nisubiri, nitawasikiliza pia kwa sababu wanahitaji kuishi pamoja kwa maelewano. Wanahitaji kupendana, kukaa katika umoja na kuwa na furaha.”

Kwa sasa, anaendesha zamu kati ya Fatuma Rafaeli, Asha Pius na Mariam John, na hutumia siku mbili na kila mmoja wao katika wiki.

Kulingana naye, anahakikisha kwamba anawapa wake wote watatu umakini wa kutosha ili kuepusha mivutano miongoni mwao.

Akisimulia kwa mara ya kwanza jinsi alivyowakutanisha, bwana Yengayenga alisema kwamba ilikuwa changamoto kwani wawili bado walikuwa kwenye chumba na wa tatu alitoka naye kijijini na kumuingiza kwenye chumba hicho hicho wakaketi wakaanza kupiga stori.

Hii hapa video ya simulizi hilo linalokwenda kwa takribani saa moja.