Mtoto wa nne? Karen Nyamu aibua maswali baada ya kuonekana kana kwamba ni mjamzito

Seneta huyo alimkaribisha mtoto wake wa mwisho, Wairimu mwezi Februari mwaka jana.

Muhtasari

•Karen Nyamu alionekana akiwa ameshikilia tumbo lake lililochomoza, na kuongeza uvumi kwamba anaweza kuwa amebeba mtoto wake wa nne.

•Picha zake zilizopigwa wikendi zilizua maswali miongoni mwa wanamitandao waliogundua tumbo lake likionekana kutokeza isivyo kawaida.

wakati wa hafla ya uzinduzi wa biashara ya Vesha Okello.
Seneta Karen Nyamu wakati wa hafla ya uzinduzi wa biashara ya Vesha Okello.
Image: JULIOH WACHIRA

Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu amewaacha watumiaji wa mitandao wakizungumza baada ya kushiriki video inayomuonyesha akionekana kuwa mjamzito.

Siku ya Jumatatu, mama huyo wa watoto watatu alichapisha video yake akiwa kwenye lifti ambapo alionekana akiwa ameshikilia tumbo lake lililochomoza, na kuongeza uvumi ambao tayari ulikuwa ukisambaa kwamba anaweza kuwa amebeba mtoto wake wa nne.

"Imekuwa muda mrefu," aliandika chini ya video hiyo.

Hata hivyo hakushiriki maelezo zaidi vesha okellopkuhusu video hiyo. Pia haijulikani ikiwa video hiyo ni ya sasa au ni video ya zamani. Je, seneta huyo wa UDA anaweza kuwa na mimba ya mtoto mwingine, mwaka mmoja tu baada ya kujifungua mtoto wake wa tatu?

Picha zake zilizopigwa wakati wa uzinduzi wa biashara ya bintiye Akothee, Vesha Okello, siku ya Jumamosi jioni tayari zilikuwa zimezua maswali miongoni mwa wanamitandao ambao waligundua tumbo lake likionekana kutokeza isivyo kawaida.

Kundi kubwa la wanamitandao ambao walitoa maoni kuhusu picha za mwanasiasa huyo asiyepungukiwa na drama maishani zilizosambazwa na Mpasho walidai kuwa alionekana wazi kuwa ni mjamzito.

Serah Kabz Mwangi: Jehova.. Mimba ya tatu

Shirleen Osundwa Otengo: Karen Nyamu ako na bol kwani?

Nyambura Kanyi: Samidoh amefanya ile kitu tena

Liliane Ndush Nzilani: Hii tumbo ya Mama Wairimu inasemaje?

Margaret Joe: Karenzo ako na ball ingine ama ni macho yangu iko na shida?

Karen Nyamu ni mama wa watoto watatu, wasichana wawili na mvulana mmoja. Alipata watoto wawili wa mwisho na mpenzi wake mwimbaji maarufu wa nyimbo za Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh huku mtoto wake wa kwanza akitoka kwa mahusiano yake na mcheza santuri maarufu wa Kenya, DJ Saint.

Seneta huyo wa kuteuliwa alimkaribisha mtoto wake wa mwisho, Wairimu mnamo mwezi Februari mwaka jana.

Image: INSTAGRAM/// KAREN NYAMU