Mke amuuwa mumewe kisha awa mstari wa mbele kumuomboleza kwa uchungu na jitimai

Inadaiwa alishirikiana na wanawe kumvamia na kumpiga mumewe hadi kufa baada ya kuchelewa kurudisha gari ambalo alitaka kutumia kufika nyumbani kutoka kwa rafiki yake. Ama kwa kweli, ogopa wanawake!

Muhtasari

•Mke huyo alikwenda hadi kwenye Facebook na kumuandikia mumewe ujumbe wa kumuomboleza akiuliza Mungu maswali kwa nini alifariki.

• Lakini uchunguzi wa maiti baada ya kufukuliwa ulionesha mwanamume huyo alipigwa na kuvunjwa nyumbani.

Mwili wa marehemu
Mwili wa marehemu
Image: Instagram//Azam

Mwanamke mmoja kwenye mtandao wa Facebook amegeuzwa kicheko na mtu wa kutupiwa maneno ya kila rangi baada ya kubainika kwamba ndiye alimuuwa mume wake lakini kwenda kwenye mtandao huo kuachia ujumbe mrefu wenye machungu akiomboleza kifo chake.

Mwanamke huyo kwa jina Mwila Kasase alimuomboleza mumewe kwenye ukurasa wa Facebook wakati alifariki, lakini baada ya kuzikwa, familia ya mum wake ilimshuku na kutaka uchunguzi wa maiti kufanyika upya.

Kwa mujibu wa jarida la Zambian Observer, Inadaiwa alishirikiana na wanawe kumvamia na kumpiga mumewe hadi kufa baada ya kuchelewa kurudisha gari ambalo alitaka kutumia kufika nyumbani kutoka kwa rafiki yake.

Mwili wa marehemu hata ulizikwa lakini familia yake ilisisitiza kufanyiwa uchunguzi wa maiti kwa sababu walishuku mchezo mchafu.

Mwili huo ulitolewa na kuchunguzwa siku ya Jumatano na matokeo ya uchunguzi yalionyesha kuwa mtu huyo alivunjika mkono, mguu na mbavu.

Lakini wakati wa mazishi, alilia zaidi na hata akaenda kwenye mitandao ya kijamii kuhoji Mungu kwa nini aliruhusu mumewe afe.

“Mume wangu, hili limenivunja moyo kwa sana, Mungu wangu mbona ukaruhusu mume wangu kufa? Nimeishiwa maneno, hata sijui jinsi nilimuomboleza,” sehemu ya ujumbe wake ilisoma.

mauaji
mauaji

Inaarifiwa baada ya matokeo hayo ya uchunguzi wa maiti kubaini kuwa marehemu alipigwa, mke na wanawe walikuwa washukiwa wa kwanza na walikiri kumpiga hadi kusababisha kifo chake.