Mahaba huku Karen Nyamu akimsindikiza Samidoh hadi uwanja wa ndege akielekea China

Seneta Nyamu alimtakia wakati mwema baba huyo wa watoto wake wawili wadogo wakati akiwa China.

Muhtasari

•Samidoh alifichua kuhusu kuwasili kwake katika jiji la Guangzhou nchini China siku ya Ijumaa alasiri kwa taarifa ya vichekesho.

•Alipopanda eskaleta, staa huyo wa Mugithi alionekana akituma mabusu kwa mpenzi wake, seneta Nyamu.

nchini kuelekea Uchina.
Samidoh aliondoka nchini kuelekea Uchina.
Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Mwimbaji maarufu wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh yuko nchini China kwa ziara ya kikazi kwa muda ambao haujathibitishwa.

Baba huyo wa watoto watano alifichua kuhusu kuwasili kwake katika jiji la Guangzhou nchini China siku ya Ijumaa alasiri kwa taarifa ya vichekesho.

"Kupotea Uchina: Najaribu kutofautisha ishara za barabarani na bidhaa kwenye menyu, lakini nimeshinda kabisa kwa sura ya 'msafiri aliyechanganyikiwa," Samidoh aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Wakati alipokuwa akiondoka nchini kuelekea nchi hiyo ya bara Asia, Samidoh aliandamana na mpenzi wake Karen Nyamu hadi uwanja wa ndege na seneta huyo wa kuteuliwa alionyesha video za mwimbaji huyo ambazo alipiga alipokuwa akimuaga.

Kwenye maelezo ya video hizo zilizoshirikiwa Ijumaa asubuhi, Nyamu alimtakia wakati mwema baba huyo wa watoto wake wawili wadogo akiwa China.

“China, tafadhali mtunze baba Nimu @samidoh.muchoki,” Karen Nyamu aliandika kwenye mojawapo ya video hizo.

Katika video nyingine, Samidoh alionekana akitembea kwenye korido za uwanja wa ndege huku akiwa amebeba gitaa lake mgongoni. Alikuwa ameandamana sako kwa bako na mwanamke mwingine asiyetambulishwa.

Kabla ya kupanda eskaleta, staa huyo wa Mugithi alionekana akituma mabusu kwa Karen Nyamu. Samidoh pia alishiriki upya video iliyochapishwa na mpenziwe kwenye ukurasa wake kama ishara ya kumthamini mwanasiasa huyo.

Mwezi uliopita, Karen alifichua kwamba amekuwa kwenye mahusiano naSamidoh kwa takriban miaka mitano.

Katika mahojiano na Ala C kwenye kipindi cha Reke Ciume na Ene, mama huyo wa watoto watatu alifichua kwamba alikutana na baba huyo wa watoto wake wawili wadogo katika shughuli za kisiasa.

Hata hivyo, alikanusha madai kwamba waliunganishwa pamoja na mfanyibiashara Mike Sonko kama alivyodai gavana huyo wa zamani wa Nairobi katika siku za nyuma. 

"Sonko alidhani hivyo (alikuwa ametuunganisha), lakini hata wakati ule tukiwa Dubai tulikuwa tunajuana. Sonko alikuwa bosi wangu, nililazimika kumficha white. Nilikuwa nimeficha white kwa hiyo alidhani yeye ndiye aliyefanya hivyo, kumbe tulikuwa tumezungumza (na Samidoh)," Nyamu alisema.

Seneta huyo wa UDA pia alikanusha madai ya kuvunja ndoa ya Samidoh na ya 'kumuiba' mwimbaji huyo wa Mugithi kutoka kwa mkewe wa miaka mingi, Edday Nderitu.

“Sijawahi kumuibia mtu mume, tena huyo mwanaume, nina watoto naye na anapenda watoto. Ukitaka kugombana na kutofautiana naye, jaribu kumtenga na watoto wake, wote,” alisema.

Nyamu alidokeza kuwa mzazi mwenzake ameweza kutunza nyumba zake zote mbili, yake na ya Edday Nderitu kwa miaka mingi.