Vera atoa onyo kali kufuatia ripoti isiyo sahihi ya Edgar Obare kuhusu safari yake ya Dubai

Edgar alidai kuwa safari ya Vera imefadhiliwa na tajiri wa Kirusi ambaye alipaswa kukutana naye jijini Jumeirah.

Muhtasari

• Edgar Obare amelazimika kuomba msamaha baada ya kuripoti vibaya kuhusu safari ya Dubai ya mwanasosholaiti Vera Sidika.

•Vera alidokeza kuwa kuendelea, wanablogu wanaosema uongo kumhusu watajipata katika hatari ya kufikishwa mahakamani.

ametoa onyo baada ya Edgar Obare kuandika ripoti isiyo sahihi kuhusu safari yake ya Dubai.
Vera Sidika ametoa onyo baada ya Edgar Obare kuandika ripoti isiyo sahihi kuhusu safari yake ya Dubai.
Image: INSTAGRAM//

Mwanablogu maarufu Edgar Obare amelazimika kuomba msamaha baada ya kuripoti vibaya kuhusu safari ya Dubai ya mwanasosholaiti Vera Sidika.

Wikendi, mwanablogu huyo alidai kuwa safari ya Vera imefadhiliwa na tajiri wa Kirusi ambaye alipaswa kukutana naye jijini Jumeirah.

"Chanzo kinadai kuwa mama wa watoto wawili, Vera Shikwekwe, alisafiri kwa ndege hadi Dubai kuungana na tajiri wake wa Urusi aliyeoa katika Jumeirah na kudai kutohudumiwa na wafanyikazi wa Afrika Mashariki kwa kuwa yeye ni mtu mashuhuri. Brown Mauzo hatakiwi kuona haya," Edgar Obare aliripoti Jumamosi.

Siku moja tu baadaye, mwanablogu huyo mashuhuri alibatilisha ripoti yake ya awali na kufichua kwamba Vera alikuwa amejibu na kutoa ukweli.

Katika taarifa ya Jumapili, Edgar aliomba msamaha kwa kejeli kwa mama huyo wa watoto wawili akikiri kwamba ripoti ya awali haikuwa sahihi.

"Tunaomba radhi kwa ripoti isiyo sahihi ya safari ya Dubai ya mwanasosholaiti Vera Sidika kufadhiliwa na mbwenyenye wa Kirusi, alijibu na kutupa risiti," mwanablogu huyo aliandika kwenye Instagram.

Kupitia ukurasa wake, Vera alithibitisha kukubali msamaha wa mwanablogu huyo na kumshauri dhidi ya kuandika habari zisizo sahihi kumhusu katika siku zijazo.

"Msamaha umekubaliwa. Hebu turekebishe uandishi wa stori kulingana na ukweli na uthibitisho na risiti. Sio tetesi kutoka kwa akaunti za uwongo za watu wasionipenda," Vera aliandika.

Mke huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo aliendelea kutuma onyo kwa wanablogu wote akiwaonya dhidi ya kuandika uwongo kumhusu.

Alidokeza kuwa kusonga mbele, wanablogu wanaosema uongo kumhusu watajipata katika hatari ya kufikishwa mahakamani.

"Kuanzia leo, Blogu yoyote inayoniandikia habari za uongo na uzushi, bora uwe na uthibitisho wa madai au tunaenda mahakamani. Hiyo ni mwisho. Ni Vera Sidika 2.0. Sichezi muda huu," sema.

Mama huyo wa watoto wawili alidokeza zaidi kuwa hatapuuza tena hadithi ghushi zinazoandikwa kumhusu na kuonya kuwa watu wanaojihusisha nazo watajiingiza kwenye matatizo naye.