Dokta mrembo na tajiri wa miaka 40 alia na kujuta kuwakataa wavulana enzi za ujana wake

Daktari huyo wa masuala ya kifamilia alisema kwamba baada ya kuhitimu miaka 40 bila kuwa na mtoto wala mpenzi, amenaza kuingiwa na wasiwasi wa kukosa amani katika nafsi yake.

Muhtasari

• Alishiriki nyakati zake za kutojiamini, akikiri waziwazi kuwa na hali ya kutokamilika.

Screengrab
Screengrab

Katika video mbichi na ya kipekee iliyoshirikiwa kwenye akaunti yake ya Facebook, Dkt. Jen Caudle, daktari maarufu wa familia anayeishi Philadelphia, Marekani, alifungua dirisha la maisha yake, akifichua furaha na vikwazo vya kuwa mwanamke mseja zaidi ya miaka 40 bila mwenzi au watoto.

Video hiyo, ambayo imewavutia watazamaji wengi iliangazia mapambano anayokumbana nayo huku ikikumbatia safari yake ya kipekee na shinikizo za kijamii ambazo zinaweza kuweka kivuli kwenye mafanikio yake.

Dk. Caudle, ambaye amepata heshima na kutambuliwa kwa utaalamu wake wa matibabu, alichagua kuchukua njia ya wazi ili kushiriki mawazo na uzoefu wake.

Video hiyo ya dhati iligusa hofu yake ya kuwa mseja na hamu ya uhusiano wa kina ambao unaweza kuishia katika kitu kizuri kama ndoa.

"Hii ni mada ambayo kwa muda mrefu imekuwa nyeti sana, na kama nikiwa mdogo ningejua kwamba siku moja ningekuja kuanza kuzungumzia kuhusu kutoolewa na tayari nimefika miaka 40 nafikiri ningeudhika kwa kuwa ni suala la nyeti kwa kweli..." Daktari huyo alianza.

Unyoofu wake tangu wakati huo umevutia wafuasi wake, na kuonyesha kwamba udhaifu unaweza kufungua njia kwa mazungumzo ya maana kuhusu magumu ya maisha.

Daktari huyo wa familia hakusita kukiri changamoto anazokabiliana nazo alipolinganisha maisha yake na ya wenzake walioolewa ambao wana watoto.

Alishiriki nyakati zake za kutojiamini, akikiri waziwazi kuwa na hali ya kutokamilika katika muktadha wa kanuni za kijamii ambazo mara nyingi hulinganisha utimilifu wa kibinafsi na hatua muhimu za jadi.

"Unajua sijawahii kuwa na mtoto na suala kuhusu kupata mtoto kwanza kwa mwanamke ambaye umeshafikisha miaka 40 kwenda juu huwa halina mashiko. Kwa muda mrefu nimekuwa na mashaka kuhusu ni nini watu watasema kuhusu mimi kuwa na miaka 40 bila mume wala watoto, jamii nyingi huangalia watu kwa njia hiyo," alisema.

Kupitia video yake, Dkt Caudle alionyesha kwamba hata watu waliokamilika hukabiliana na mashaka na kutokuwa na uhakika ambao unaweza kutokana na matarajio ya jamii.

Tazama video hii hapa;