"Kuna ubaya gani?" Akothee azungumzia madai ya Ababu Namwamba kutoka kimapenzi na Azziad

Akothee alifichua kwamba alimpigia simu Azziad kuhusu suala hilo wakati maji yalipozidi unga.

Muhtasari

•Akothee alimbainishia Azziad kwamba hakuna tatizo yeye kuchumbiana na waziri Namwamba ikiwa wote wawili hawako katika mahusiano mengine.

•Akothee alishangaa ni kwa nini Wakenya wanafanya uhusiano unaodaiwa kuwa kati ya wawili hao kuwa suala kubwa.

Azziad Nasenya na Ababu Namwamba
Image: HISANI

Mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee ametoa taarifa kuhusu uvumi ambao umekuwepo kwa muda wa madai ya mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanahabari Azziad Nasenya na waziri Ababu Namwamba.

Katika taarifa ya Jumatatu asubuhi, mama huyo wa watoto watano alifichua kwamba alimpigia simu Azziad kuhusu suala hilo wakati maji yalipozidi unga.

Wakati wa mazungumzo yao, Akothee alimbainishia mwanatiktok huyo mwenye umri wa miaka 23 kwamba hakuna tatizo lolote yeye kuchumbiana na waziri Namwamba ikiwa wote wawili hawako katika mahusiano mengine.

"Nimetangamana na wote wawili (Azziad & Ababu). AZZIAD ni kama binti yangu. Mambo yalipokaa nilimtafuta. Alisema hajui ni kwa nini Wakenya walimhusisha na Waziri na maneno yangu kwake yalikuwa, ‘Mummy, na kuna ubaya gani kuchumbiana na CS ikiwa hajaoa na yuko tayari kuchumbiana?’ Nikamwambia ukimpenda na anakupenda, endea hilo, kwani ni kesho," Akothee alisema kupitia Instagram.

Katika majibu yake kwa Akothee, Azziad hata hivyo alidokeza kuwa hakuna chochote kabisa kinachoendelea kati yake na waziri huyo wa michezo

"Hapana mama, hatuna chochote, kwa sasa ninafanya kazi yangu," Azziad alimjibu mwanamuziki huyo.

Mwanamuziki huyo alishangaa ni kwa nini Wakenya wanafanya uhusiano unaodaiwa kuwa kati ya wawili hao kuwa suala kubwa huku akibainisha kuwa wote ni watu wazima wanaohitimu kuchumbiana sasa.

Alidokeza kuwa kuna maswala mengine mengi ambayo yanahitaji kushughulikiwa kando na madai ya uhusiano kati ya waziri Namwamba na Azziad.

“Hiki hakiwezi kuwa kichwa cha habari cha kila siku. Tuna masuala mazito zaidi ya kuhudhuria pia. Na tukiendelea, nani anadai AZZIAD na nani anamdai waziri? Shida kubwa mbali na kula calamari na mvinyo wa bei ghali nilisikia juzi bungeni?” alihoji.

Aliongeza, “Wakenya, tuna tembo wakubwa chumbani mbali na masuala ya chumba cha kulala. Nimeenda mimi. Iwafikie.

AKOTHEE KENYA on Instagram: "Well I just feel like causing trouble before I leave Kenya Let me ask one question 1. Is Azziad not over 18? 2. Is she not a woman enough to date ? 3. Is The CS Ababu.a not A man enough ? A luhya African Man for that sake ( you know what I mean ,I mean If he had a wife or whatever he can still do his shit just like Most African men do 4. Azziad has never declared to be anyone's wife , She is just but a child , KENYANS ,AZZIAD IS A BABY PLEASE 😭😭. Not your competition. Ohh yes I have interacted with both of them. AZZIAD is like my daughter, When things Got tight I reached out to her , She has no idea why Kenyans plant The CS on her and my words to her "Mummy ,and what is wrong by dating the CS if he is single and ready to mingle, I told her if you like him. & He likes you Go for it kwani ni kesho" .her words "No mommy, we have nothing, Currently I am working on my career" ,as A mother I feel Kenyans are becoming too much . This can't be the daily headline. We have more serious issues to attend too. And by the way Who is claiming AZZIAD and who is claiming the CS ? Shida kubwa apart from Eating calamary and Expensive wine nillisikia juzi kwa parliament ni gani ? As a rejected committee member of talanta hela . I ask Kenyans to be sober , avoid side shows and address the Elephant in the room . As the creatives before we were revoked,we gave out a proper 5 years road map and execution plan for the creative industry. I personally made sure MCSK got their license,which was stuck for years under KECOBO to collect as much revenue as possible and support the suffering Artists . KENYAAANS WE HAVE BIG ELEPHANTS IN THE ROOM APART FROM BEDROOM IISSUES nimeenda mimi Iwafikie. When your man is over the moon about this , AZZIAD is his crash , when your woman makes this topic of discussion, she is crashing on mheshimiwa period Kila mtu apambane"

Wiki jana, Waziri Ababu Namwamba katika mahojiano alizima tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Azziad Nasenya.

Katika mahojiano, Waziri huyo alisema wawili hao hawana uhusiano wowote.

"Hapana. Azziad si mpenzi wangu. Kwa kweli ninajisikia vibaya sana na ninamsikitikia msichana maskini," Ababu alisema.

Aliongeza, "Unajua mimi nimekuwa kwenye siasa sana na unapofanya kazi kwenye maeneo ya umma unapata ngozi ya mamba, iliyofunikwa na kiboko iliyofunikwa na ngozi ya nyati. Watu ambao hawajazunguka katika nafasi hii wanapitia."