Siku yenye furaha zaidi maishani mwangu-Shakilla afurahia kutengana kwa Vera Sidika na Brown Mauzo

Lakini katika hali hiyo mwanasosholaiti Shakilla anaonekana kufurahishwa na kutengana kwa wawili hao.

Muhtasari
  • Lakini katika hali hiyo mwanasosholaiti Shakilla anaonekana kufurahishwa na kutengana kwa wawili hao.
  • Mwanamuziki huyo aliendelea kumshukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.
Shakilla amshambulia Vera Sidika, Brown Mauzo atajwa
Shakilla amshambulia Vera Sidika, Brown Mauzo atajwa
Image: Instagram

Msanii Brown Mauzo na mwanasosholaiti na mama wa watoto wake 2 Vera Sidika siku ya Jumatano kupitia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii walitangaza kutengana kwao.

Habari hizi ziliwafikia na kuwapata wafuasi wao kwa mshtuko.

Lakini katika hali hiyo mwanasosholaiti Shakilla anaonekana kufurahishwa na kutengana kwa wawili hao.

Kupitia kwenye Insta stories zake alimshambulia Vera huku akidai kwamba alijua kwamba ni yeye mwenye shida kwenye uhusiano huo.

Pia alitangaza kuwa hii ndio siku yenye furaha zaidi maishani mwake;

Huku niki nukuu ujumbe wake alisema;

"Hii ndio siku yenye furaha zaidi maishani mwangu,nilijua wewe ndio ulikuwan shida mpaka Brown Mauzo anakuacha sijui unataka kurejea mitaa gani, lakini natumai sio yangu,"Shakilla aliandika.

Kwa upande wake Brown Mauzo alisema;

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Brown Mauzo alitangaza Jumatano.

Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Mwanamuziki huyo aliendelea kumshukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

 “Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"

Mauzo alidokeza kuwa ukurasa  unaofuata wa maisha yao utakuwa kuhsu uponyaji wa moyo baada ya kuachana na kukumbatia yake yaliyo mbele.

"Ingawa sehemu zetu zinaweza kutofautiana, tutathamini kumbukumbu ambazo tumeunda pamoja. Sote tunasalia kushukuru kwa masomo tuliyojifunza na ukuzi ambao tumepitia. Lengo letu sasa ni uponyaji na kukumbatia siku zijazo kwa mioyo iliyo wazi. Asanteni kwa mara nyingine tena kwa kuwa sehemu ya safari yetu,” alisema.

Saa moja baadaye, Vera alishiriki picha zake akiwa ndani ya ndege inayoelekea mahali ambapo aliwaacha mashabiki wake wakisie tu.