"Usicatch feelings!" Vera Sidika avunja kimya baada ya Brown Mauzo kutangaza wameachana

Vera ameonekana kutupa vijembe muda mfupi baada ya mzazi mwenzake Brown Mauzo kutangaza wameamua kutengana.

Muhtasari

•Brown Mauzo kupitia mitandao ya kijamii alitangaza kuwa wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

•Vera alionekana kutosumbuliwa wala kutikiswa na chochote alipokuwa amejistarehesha kwenye sehemu ya kifahari ya ndege.

amevunja kimya baada ya Brown Mauzo kutangaza wameachana.
Vera Sidika amevunja kimya baada ya Brown Mauzo kutangaza wameachana.
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti wa Kenya Vera Sidika amejibu kwa ujumbe wa kimafumbo muda mfupi baada ya mzazi mwenzake Brown Mauzo kutangaza kuwa wameachana.

Siku ya Jumatano, Brown Mauzo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii alitangaza kuwa wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Brown Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Mwanamuziki huyo aliendelea kumshukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

 “Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"

Mauzo alidokeza kuwa ukurasa  unaofuata wa maisha yao utakuwa kuhsu uponyaji wa moyo baada ya kuachana na kukumbatia yake yaliyo mbele.

"Ingawa sehemu zetu zinaweza kutofautiana, tutathamini kumbukumbu ambazo tumeunda pamoja. Sote tunasalia kushukuru kwa masomo tuliyojifunza na ukuzi ambao tumepitia. Lengo letu sasa ni uponyaji na kukumbatia siku zijazo kwa mioyo iliyo wazi. Asanteni kwa mara nyingine tena kwa kuwa sehemu ya safari yetu,” alisema.

Saa moja baadaye, Vera alishiriki picha zake akiwa ndani ya ndege inayoelekea mahali ambapo aliwaacha mashabiki wake wakisie tu.

Katika picha hizo, mama huyo wa watoto wawili alionekana kutosumbuliwa wala kutikiswa na chochote alipokuwa amejistarehesha kwenye sehemu ya kifahari ya ndege.

"Catch flights, not feelings, Guess my next stop," Vera alisema na kuandamana na ujumbe wake wenye emoji ya ndege inayosonga.

Kumaanisha: Chukua safari za ndege, sio hisia, Kisia nitakakosiamama tena.

Vera na Mauzo wamekuwa pamoja kwa takriban miaka mitatu na tayari wawili hao wana watoto wawili pamoja, mvulana na msichana.