Mwanamke arekodiwa 'akimpiga' afisa wa kampuni ya maji kwa kumkatia maji - Video

Afisa huyo asiyejiweza anaonekana kwenye video akihangaika bila matunda kujinasua kutoka kwa mshiko thabiti wa mwanamke huyo huku akiapa kutomuunganisha tena kwenye mfumo wa usambazaji maji.

Muhtasari

• Baadhi ya watu waliokuwa karibu wanaonekana wakijaribu kuingilia kati na kumsihi mwanamke huyo amwachie afisa huyo.

Mwanamke akimpiga mwanamume
Mwanamke akimpiga mwanamume
Image: Instagram

Video moja imebuka mitandaoni ikimuonesha mwanamke mmoja alimdhalilisha wazi wazi mwanamume mmoja kwa kumkunja mashati huku watu wakishangilia.

Kwa mujibu wa blogu moja kutoka nchini Ghana, iliarifiwa kwamba mwanamume huyo aliyeonekana akikunjwa mashati ni mfanyikazi katika kamouni ya maji na alikuwa anadhalilishwa kwa madai kwamba alimkatia mwanamke huyo maji kwa kutolipa bili ya maji.

Video ya mwanamke huyo mwenye hasira akiwa amemshika afisa huyo kwenye eneo la shingo la shati lake la mikono mirefu, na kumburuta huku kukiwa na amri ya kumfungulia maji.

Afisa huyo asiyejiweza anaonekana kwenye video akihangaika bila matunda kujinasua kutoka kwa mshiko thabiti wa mwanamke huyo huku akiapa kutomuunganisha tena kwenye mfumo wa usambazaji maji.

Baadhi ya watu waliokuwa karibu wanaonekana wakijaribu kuingilia kati na kumsihi mwanamke huyo amwachie afisa huyo, lakini hakutaka kutetereka, badala yake, aliapa kutomtoa mikononi mwake hadi atakapomrudishia maji.

Video hiyo imezua hisia tofauti, huku baadhi ya Waghana wakilaani tabia ya mwanamke huyo na kutaka akamatwe na kufunguliwa mashitaka, huku wengine wakisema inawahudumia wafanyakazi wa GWC ipasavyo kwa sababu wanadaiwa kujulikana kwa kuwatendea vibaya wateja.

Tazama video hiyo hapa chini;