Upasuaji wa kurembesha uso waenda mrama, mrembo abadilika kama mtu aliyepigwa - Video

Mchapishaji wa video hiyo alisema kwamba mrembo huyo alitaka kufanya maboresho katika muonekano wa uso wake ili kumvutia mwanamume aliyekuwa anamtaka.

Muhtasari

• Watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wamekumbana na video hiyo wamemkashifu bibi huyo kwa kutoridhika na uso ambao Mungu alimbariki nao.

• Na katika kujaribu kuthibitisha kuwa yeye ni mwenye busara kuliko muumbaji, ameachwa na uso usiotambulika.

Mrembo alaiyefanyiwa upasuaji wa uso.
Mrembo alaiyefanyiwa upasuaji wa uso.
Image: Instagram

Mrembo mmoja amesalia na uso uliobadilika kwa njia hasi baada ya upasuaji wa kuongeza urembo usoni kugeuka na kuwa chanzo cha matatizo yake.

Katika video moja ambayo imepakiwa na blogu ya nchini Ghana, mrembo huyo ambaye alisemekana kuendea upasuaji wa kuongeza urembo wake upande wa uso alirejea akiwa amevimba kwa mbali utadhani ni bondia anayetoka kwenye mduara baada ya kuoneshwa kivumbi kwa ngumi za mpinzani.

Mrembo huyo alionekana amevimba uso kwa njia ya kutia huruma huku mtu aliyeonekana kama daktari akiendelea kumpa huduma kwa kumtibu uso wake katika harakati ya kujaribu kuokoa sura yake kabla ya kuharibika Zaidi.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wamekumbana na video hiyo wamemkashifu bibi huyo kwa kutoridhika na uso ambao Mungu alimbariki nao.

Na katika kujaribu kuthibitisha kuwa yeye ni mwenye busara kuliko muumbaji, ameachwa na uso usiotambulika.

Mchapishaji wa video hiyo aliandika kuwa mrembo huyo huenda alimezwa na shinikizo kutoka kwa wanaume ambao wanaweka vigezo na vikwazo vingi kwa wanawake ambao wangependelea kutoka nao kimapenzi au labda kuoana nao.

“Kutoka BBL hadi kwa uboreshaji wa uso (Upasuaji) yote haya ili kumvutia mwanaume ambaye atakupa moyo uliovunjika. Wanawake wanapitia mengi 😢 💔🙆.” Chapisho hilo lilisoma.

Hapo chini ni baadhi ya maoni yaliyokusanywa chini ya video iliyoenea…

“Si mara zote kufanya kwa ajili ya mwanamume, wakati mwingine unahitaji kujiamini wewe mwenyewe na kujikubali,” mmoja alisema.

“Nilidhani alikuwa anatoka tu kwenye Uwanja wa ndondi,” mwingine alidhania.

“Mungu anipitishe mbali na shinikizo kama hili 😂😂😂😂. Sio kikombe changu cha chai 🍵. Nihesabu nje mimi 😂😂😂” mrembo alisema.