Mrembo agundua mama wa boyfriend si mamake bali ni bosi baada ya kumuoshea vyombo

"Pindi baada ya kufika kule, nilianza kuosha vyombo, kupakulia wageni chakula na kusalimia kila mtu kama ‘mke mpya kwenye boma’. Wiki chache baadae, niligundua walimpa kazi ya kutafuta mtu wa kupakulia wageni.”

Muhtasari

• Kwa maana nyingine, alichokifanya ni kumsaidia mpenzi wake kufanya kazi ambayo yeye mwenyewe alikuwa ameratibiwa kufanya.

Mwanamke mwenye huzuni
Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Mrembo mmoja amewashangaza watu katika mitandao ya kijamii baada ya kusimulia kitendo cha ajabu na cha aibu ambacho kilisababisha kuvunja uhusiano wake na aliyekuwa mpenzi wake.

Katika ujumbe huo ambao umekuwa ukienezwa mitandaoni, watu walikuwa wanaelezea matukio ambayo hawawezi kuyasahau ambayo yalipelekea kuvunjika kwa uhusiano wao wa kimapenzi.

Mrembo huyo alisimulia kwamba alikuwa na mpenzi wa kiume ambaye alimualika siku moja kwenda kwao kukutana na familia yake wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mama yake.

Mrembo alipofika kwa kina mpenzi, mpenzi huyo alimwambia kwamba angehitaji kumfurahisha mama yake kwa kufanya kazi za ndani chapchap kama kung’arisha boma, kupika, kuosha vyombo na majukumu mengine ambayo aghalabu kutekelezwa na wanawake.

Alisema kwamba alimtaka kufanya hivyo kama njia moja ya kumfurahisha mama mtu ili kumkubalia kumuoa na kumleta nyumbani kama mke rasmi.

Mrembo huyo alielezea kwamba baadae alikuja kupigwa na butwaa alipogundua kwamba yule mama ambaye aliambiwa amfurahishe kwa kumfanyia kazi za ndani siku yake ya kuzaliwa hakuwa mama wa mpenzi wake.

Alisema kwamba aligundua mama yule alikuwa ni bosi wa mpenzi wake na kuwa mpenzi huyo wake alikuwa ameajiriwa katika boma lile kama kijakazi. Kwa maana nyingine, alichokifanya ni kumsaidia mpenzi wake kufanya kazi ambayo yeye mwenyewe alikuwa ameratibiwa kufanya.

“Mpenzi wangu [wa kipindi hicho] alinialika katika tafrija ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mamake aliyekuwa akifikisha miaka 50. Aliniambia ‘nimfurahishe mamake’. Pindi baada ya kufika kule, nilianza kuosha vyombo, kupakulia wageni chakula na kusalimia kila mtu kama ‘mke mpya kwenye boma’. Wiki chache baadae, niligundua kwamba mpenzi wangu hakuwa anahusiana kinasaba na mtu yeyote katika boma lile. Walimpa kazi ya kutafuta mtu wa kusaidia katika tafrija,” ujumbe huo ulisoma.

Mrmbo kuomba ushauri,mama mkwe,
Mrmbo kuomba ushauri,mama mkwe,

Watu walikuwa na maoni ya kushangaza wengine wakimcheka na wengine wakiwataka warembo kufanya uchunguzi wa kina kwa wale wazazi ambao wapenzi wao wanawatambulisha kwao huenda wakawa ni wa kupanga.

"Wakati mwingine nyie wanawake mnajitolea kutumiwa 😏Kumvutia Mama yake kama vipi?Unaweza kuwa umevaa vizuri zaidi ili kuthibitisha kuwa ni maalum yake badala ya kazi hiyo duni" Khimmy Doncs aliuliza.