Jimal Rohosafi ajibu kuhusu aliyekuwa mke wake, Amira kutoka kimapenzi na mwanaume mwingine

Amira amekuwa akimuonyesha waziwazi mpenzi wake mpya na kubainisha kuwa ana furaha katika mahusiano yake mapya.

Muhtasari

•Mwanamtandao alimchokoza Jimal kwa kumuuliza ikiwa anajua kwamba mke wake wa zamani anachumbiana na mwanamume mwingine.

•Baba huyo wa watoto wawili alijibu kwa kejeli, "Ndio, lakini na wewe kuwa busy kwa DM zangu pls."

amejibu swali kuhusu Amira kupata mpenzi mpya.
Jimal Rohosafi amejibu swali kuhusu Amira kupata mpenzi mpya.
Image: HISANI

Mfanyabiashara maarufu Jimal Marlow Rohosafi alijibu kwa kejeli na ukali baada ya kuulizwa ikiwa anafahamu kuwa mke wake wa zamani Amira tayari amenyakuliwa na mwingine.

Amira ambaye alitalikiana rasmi na baba huyo wa watoto wake wawili mwaka jana katika siku za hivi majuzi amekuwa akimuonyesha waziwazi mpenzi wake mpya kwenye mitandao ya kijamii na kudokeza kuwa ana furaha katika uhusiano wake mpya.

Siku ya Jumatatu, mtumiaji wa Instagram alimchokoza Jimal kwa kumuuliza ikiwa anajua kwamba mke wake wa zamani anachumbiana na mwanamume mwingine.

Amira alipata mtu umeskia izo?” @annshiks722 alimuuliza mfanyabiashara huyo.

Baba huyo wa watoto wawili alijibu kwa kejeli, "Ndio, lakini na wewe kuwa busy kwa DM zangu pls."

Image: INSTAGRAM// JIMAL ROHOSAFI

Katika wiki moja iliyopita, Amira ambaye ana watoto wawili na mfanyabiashara huyo wa matatu amekuwa akimuonyesha mpenzi wake mpya kwenye mitandao ya kijamii.

Ingawa hakuna mengi yanayojulikana hadharani kuhusu mwanaume huyo mpya katika moyo wa Amira, imebainika kuwa anajitambulisha kama @osellunyalik kwenye mtandao wa Instagram na anaonekana kuwa mhandisi kitaaluma. Ni dhahiri kuwa licha ya kuwa Mkenya, mwanamume huyo pia anaishi Austria, Norway na Uingereza.

Wapenzi hao katika siku za hivi majuzi wamekuwa wakifurahia muda katika eneo la  Pwani na Amira ameonyesha wazi kuwa ameridhika sana na mpenzi wake mpya.

"Na mbona hamkuwa mmeniambia mapema mapenzi ya kiluo inakuwa nzuri hivi," Amira alisema siku ya Jumatatu.

Haya yanajiri takriban miaka miwili baada ya mfanyibiashara huyo wa vipondozi kugura ndoa yake na Jimal Rohosafi.

Julai mwaka jana, Jimal alijaribu kumuomba radhi mama huyo wa watoto wake kwa drama nyingi alizosababisha kwenye ndoa yao mwaka 2021.

Katika ombi lake, Jimal alikiri kuwa alimkosea sana mkewe kwa kutekeleza wajibu wake wa kumlinda. Alimuomba Amira apokee ombi lake la msamaha huku akimkumbusha jinsi ambavyo wamepitia mengi pamoja.

"Ilikuwa mbaya kabisa. Huenda nilionekana kama mtu asiye na wasiwasi lakini sikuwa na la kufanya. Nilijua haikuwa sawa, nilijua unaumia lakini sikuweza kujikusanya!Amira nafanya hivi kwa sababu ukosefu wa heshima pia ulikuwa mkubwa. Naomba radhi kwa kukosa heshima," Aliandika.

Katika jibu lake, Amira alisema hawezi kuuelewa msamaha wa mzazi mwenzake kwani ulifufua kumbukumbu ya siku mbaya za nyuma.

"Ombi hilo la msamaha limenirudisha katika sehemu moja ya giza ambayo nimewahi kuwa katika maisha yangu kwa sababu nimetafakari juu ya mengi yaliyotokea hadharani na nyuma ya milango iliyofungwa na imezua hisia nyingi," alijibu.

Mfanyibiashara huyo aliomba neema ya Mungu huku akitafakari suala hilo na kueleza kuwa kwa sasa amezidiwa na hisia.