Wasafiri wabaki vinywa wazi mhubiri akisimama na kuanza kuhubiri ndege ikiwa angani (video)

Mchungaji alikariri hitaji la abiria kumpokea Kristo na kujiweka tayari kwa ujio wa pili wa Bwana Yesu Kristo.

Muhtasari

• Kwenye video hiyo William Nishimwe alionyesha upendo wa Mungu kwa jinsi alivyoshiriki neno akiwaita waume kwa wake,wakubwa kwa wadogo kwenye toba na utakatifu.

• "Huu ni wakati wa sisi kuacha dhambi kwa sababu hukumu ya Mungu inakuja dhidi ya dhambi. Tafadhali muchukue Yesu sasa.Huu ni wakati muhimu sana kwa Yesu kama Bwana  na Mwokozi wako maana wakati umekwisha ,na Kristu Yesu anarudi."

William Nishimwe. picha;X
William Nishimwe. picha;X

Kasisi mmoja kwa jina la William Nishimwe,ameibua hisia mitandaoni baada ya kuonekana akihubiria abiria wa ndege akiwauliza wautubu dhambi.

Mchungaji huyo alishiriki video alipokuwa akitambisha neno la Mungu  na abiria wenzake waliokuwa wakisafiri kwa ndege.

Kwenye video hiyo William Nishimwe alionyesha upendo wa Mungu kwa jinsi alivyoshiriki neno akiwaita waume kwa wake,wakubwa kwa wadogo kwenye toba na utakatifu.

Aliambia abiria wakati mwafaka wa kukiri imani ni sasa kwani hukumu ya Mungu yaja.

"Huu ni wakati wa sisi kuacha dhambi kwa sababu hukumu ya Mungu inakuja dhidi ya dhambi. Tafadhali mchukue Yesu sasa. Huu ni wakati muhimu sana kwa Yesu kama Bwana  na Mwokozi wako maana wakati umekwisha ,na Kristu Yesu anarudi."

Aliendeleza mahubiri yake kwa utulivu aliopata kutoka kwa abiria,akiwaambia jinsi Yesu anavyowapenda wapendwa wake.

"Yesu anawapenda ninyi watu wa ajabu. Chukua fursa hii na uandae maisha yako." Alisema.

Mchungaji alikariri hitaji la abiria  kumpokea Kristo na kujiweka tayari kwa ujio wa pili wa Bwana Yesu Kristo.

"Bwana awabariki sana. Nilitaka tu kushiriki nanyi habari hii muhimu ili nanyi pia muweze kuandaa maisha yenu kwa ajili ya ujio wa Bwan wetu." Alisisitiza.

Hata hivyo,sio kila mtu alipoka ujumbe wake kwa furaha,huku baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wakishiriki maoni yao.

Mtumiaji anayetambulika kama @GrimdarkCthulhu alisema,

"Kulazimisha watu kusikiliza msukumo huo katika eneo ndogo kunapaswa kuwa uhalifi.Wengi hawakuwa na raha."

@moorezlife alisema, "Hakuna nji sahihi au mbaya ya kufanya hivi.Fuata tu uongozi wa Roho.wakati mwingine wanaweza kuwa sio wa kawaida."