Mrembo akosa zawadi ya gari kwa kuanguka mtihani wa kumtaja Boyfriend aliyemnunulia

Mrmbo huyo alijitetea kwamba hakutaka kuanza kutaja majina ya boyfriends ili kubahatisha na ndio maana alichagua kumtaja tu babake na akakosa gari.

Muhtasari

• Waliopewa zawadi hiyo kuikabidhi kwake walitakiwa kwanza kumuuliza swali kama la fumbo hivi ambalo iwapo angelifumbua kiufasaha basi gari lingekuwa la kwake.

Mrembo akosa gari kwa kushindwa kumtaja boyfriend
Mrembo akosa gari kwa kushindwa kumtaja boyfriend
Image: Screengrab

Mwanadada mmoja kutoka taifa jirani la Tanzania amewashangaza wengi baada ya kukosa zawadi ya gari kwa kuanguka mtihani rahisi wa kumtaja mpenzi wake aliyemnunulia.

Mrembo huyo ambaye alikuwa anafuzu kutoka chuo kikuu cha Dodoma, UDOM alitumiwa zawadi ya gari na mpenzi wake wa kiume kama njia ya kumpongeza kwa kufauli cheti cha digrii.

Ila gari hilo hakuwa analipokea kwa njia rahisi hivyo.

Waliopewa zawadi hiyo kuikabidhi kwake walitakiwa kwanza kumuuliza swali kama la fumbo hivi ambalo iwapo angelifumbua kiufasaha basi gari lingekuwa la kwake.

Alitakiwa amtaje mpenzi wake wa kiume ambaye alihisi ndiye alimnunulia gari, lakini maskini wa Mungu alihaha kati ya majina mengi ya wapenzi wake wa kiume na kumtaja mmoja ambaye alihisi kabisa ndiye mwenye uwezo wa kumnunulia gari.

Kwa bahati mbaya, aliambiwa kwamba jina la ‘Ben’ alilolitaja kama la mwanamume aliyemnunulia gari siye, na hivyo kulikosa gari lile ambalo lilirudishwa kwa mwenyewe.

Hata hivyo, baadae katika mahojiano kwenye kituo cha Clouds, Mrembo huyo alisema kwamba Ben ni babake na ndiye alihisi kabisa alimnunulia gari wala hakuwa anajua kwamab mpenzi wake angeweza kwenda hatua ya mbali hivyo ya kumnunulia gari.

“Ben ni babangu, sasa mtu aliyeniuliza nataka nini kwa siku yangu ya kuhafili nikamwambia chochote tu nitashukuru, akaniambia ananiletea Mercedes nikajua ni uongo lakini baadae nikapigiwa simu nikaambiwa nimtaje Boyfriend ndio nipewe gari, na mimi sikutaka kuanza kutaja majina ya watu, ili kuteua kitendawili nikataja jina la babangu, nikasema ni Ben, ingawa niliambiwa nimtaje boyfriend mimi nilimtaja babangu,” alijitetea kwa kukosa gari.