Amerudi soko! Justina Syokau adai kuachwa na mpenziwe

Mwanaume aliyemwona akilia alijaribu kumtia moyo aache kulia na aende nyumbani akapumzike, lakini aliendelea kulia

Muhtasari
  • Syokau alimtambulisha mwanamume wake, ambaye alisema alikuwa mfanyabiashara mjini Kisumu na hata kumshirikisha kwenye wimbo wake mpya, na kuwaacha wengi wakisema alikuwa akiwinda sana.
Image: INSTAGRAM// JUSTINA SYOKAU

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Justina Syokau yuko single kwa mara nyingine baada ya kudai kuwa tajiri wake wa Kisumu alimtupa kwenye uwanja wa ndege.

Syokau alimtambulisha mwanamume wake, ambaye alisema alikuwa mfanyabiashara mjini Kisumu na hata kumshirikisha kwenye wimbo wake mpya, na kuwaacha wengi wakisema alikuwa akiwinda sana.

Je, Justina Syokau amerejea sokoni? Hata hivyo, katika videoaliyoshiriki kwenye ukurasa wake wa facebook, mwimbaji huyo wa Twendi Twendi alionekana akilia huku watazamaji wakimtazama, akitembea bila viatu barabarani huku akiwa amebeba begi kichwani.

Kisha alisimama na kuketi wakati fulani na kudai kwamba alikuwa ametembea kwa miguu kutoka uwanja wa ndege kwa sababu inadaiwa walikuwa wakienda likizo na mume wake.

“Aliniacha kwenye uwanja wa ndege bila hela, tulikuwa tukienda mapumzikoni lakini tulipofika uwanja wa ndege alipanda ndege binafsi na kuniacha nikiwa nimekwama, akaniacha, nitawaambia nini watu bado nilikuwa najisifia. huu uhusiano kiasi hiki?Nilimwambia hata sitotoa wimbo wa 2024, akaniacha, sasa nitawaambia nini watu, aliniacha kwenye bumbuwazi,” alisema.

Mwanaume aliyemwona akilia alijaribu kumtia moyo aache kulia na aende nyumbani akapumzike, lakini aliendelea kulia

😭😭😭😭😭Billionaier aliniacha airport

Posted by Justina Syokau on Monday, December 25, 2023

Haijulikani ikiwa mwanamuziki huyo alikuwa akitafuta kiki sana kuachia wimbo wake mpya au alikuwa amevunjika moyo kweli.

Kupitia kwenye chapisho lingine msanii huyo mwenye utata aliandika ujumbe unaosoma;

"Am single again."