Samidoh amzawadi Naibu Rais Gachagua Ng'ombe

Muhtasari
  • Hivi majuzi Gachagua alikuwa miongoni mwa wageni waliohudhuria uzinduzi wa Samidoh Foundation.
NAIBU RIGATHI GACHAGUA NA MSANII WA MUGITHI SAMIDOH
Image: INSTAGRAM

Nyota wa Mugithi Samidah amemzawadia Naibu Rais Rigati Gachagua ng'ombe.

Ng'ombe huyo anaitwa Wanjiku.

Samidoh alikuwa amealikwa Mathira na Riggy G.

Katika picha, alizoshiriki kwenye ukurasa wake wa Instagram, wawili hao walionekana kutabasamu na kuwa na furaha.

"Leo alasiri niliheshimu mwaliko kutoka kwa shabiki na mshauri wangu ambaye sio mtu yeyote naibu wa rais H.E. Rigathi Gachagua, EGH katika makazi yake katika kijiji cha irúrï, Mathira na kupata fursa ya kuwaburudisha maelfu ya vijana ambao alikuwa amewaalika kwa tafrija ya Krismasi.

Pia alifichua jina la ng'ombe huyo lilichaguliwa na mkewe Naibu Rais.

"Pia nilipata fursa ya kumzawadia Wanjiku; ng'ombe wa maziwa, ambaye jina lake lilichaguliwa na Mheshimiwa Mchungaji Dorcas Rigathi."

Hivi majuzi Gachagua alikuwa miongoni mwa wageni waliohudhuria uzinduzi wa Samidoh Foundation.

Alitoa shilingi milioni moja kama sehemu ya mchango wake.