Mamake Diamond azungumzia wasiwasi kuhusu ndoa yake, aeleza kwa nini mumewe haonekani naye

Wanandoa hao wamekuwa pamoja kwa zaidi ya nusu muongo na ndoa yao haijawa laini na rahisi kila wakati.

Muhtasari

•Mama Dangote aliweka wazi hakuna mapenzi yaliyopotea na akabainisha kuwa wamepunguza kufanya mambo mengi ya kimapenzi kwa kuwa sasa wamekomaa zaidi.

•Alijivunia ndoa yake akibainisha kuwa mumewe alimuoa hata baada ya yeye kuwa na wanaume wengine hapo awali ambao hawakumuoa licha ya kuzaa nao.

Mama Dangote na Uncle Shamte
Image: HISANI

Mama mzazi wa staa wa Bongo Diamond Platnumz, Bi Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote amefunguka kuhusu kwa nini yeye na mume wake Uncle Shamte wameamua kuweka ndoa yao chini ya maji  na kuacha kuitangaza kwenye mitandao ya kijamii kama awali.

Kwa muda sasa, kumekuwa na wasiwasi kuhusu hali ya ndoa ya Mama Dangote baada ya yeye na mumewe kuacha ghafla kuonekana wakiwa pamoja kama zamani. Wawili hao ambao wamefunga ndoa rasmi wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka sita iliyopita.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na Wasafi Media, mama huyo wa bosi wa WCB aliweka wazi kuwa hakuna mapenzi yaliyopotea kati yake na Uncle Shamte na akabainisha kuwa wamepunguza kufanya mambo mengi ya kimapenzi kwa kuwa sasa wamekomaa zaidi. .

“Tushakuwa watu wazima. Mambo mengine lazima unaweka private, sio kila kitu unaweka hadharani. Kitambo ilikuwa ile wanasema, kipya kinyemi,” Mama Dangote alisema.

Aliongeza, “Zamani ilikuwa kila siku ni mapicha, manini lakini sasa tunapumzika tunaachia watoto. Unaona siku hizi watu wengi wanatuiga tu. Unaona mtu na dame yake mara wamevaa sare, mara wamevaa nini na wanaimbiana lakini sisi nambari moja tumeanza kufanya vitu hivyo. Tumeachia watoto.”

Kuhusu yeye kutoonekana na mume mdogo hadharani kama ilivyokuwa awali, Mama Dangote alieleza kuwa mpenzi wake yuko bize na kazi.

“Anauza viwanja. Ama hamjamuona kwenye viwanja?” alisema.

Mamake Diamond pia alisikika kujivunia ndoa yake naUncle Shamte akibainisha kuwa mumewe alimuoa hata baada ya yeye kuwa na wanaume wengine hapo awali ambao hawakumuoa licha ya kuzaa nao.

Wanandoa hao wamekuwa pamoja kwa zaidi ya nusu muongo na ndoa yao haijawa laini na rahisi kila wakati. Wawili hao katika siku za nyuma wameripotiwa kukosanaa na hata kutengana kwa muda mara kadhaa.