Jamaa aishiwa na nguvu baada ya kupoteza 200k kwa kamari muda mfupi baada ya kushinda

Tamaa yake ya kutaka kushinda zaidi ilimpelekea kupoteza kiasi kikubwa cha pesa ambacho alikuwa amejishindia awali kutoka kwa jukwaa hilo la mchezo wa kamari.

Muhtasari

โ€ข benbills007 alisema: "Hilo ni jambo moja kuhusu kamari ๐Ÿ˜‚..Utashinda, lakini siku watakapoenda kukusanya pesa zako zote, utalia siku hiyo ๐Ÿ˜‚."

Mcheza kamari
Mcheza kamari
Image: Screengrab//Instagram

Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo aliishiwa na nguvu na kupoteza fahamu kwa muda baada ya kupoteza laki mbili katika mchezo wa Kamari muda mfupi tu baada ya kushinda pesa hizo kutoka kwa mchezo huo huo wa Kamari.

Kwa mujibu wa blogu ya GossipMill iliyochapisha hadithi hiyo, mwanamume huyo alibahatika kushinda mchezo wa Kamari na kupata Naira laki mbili lakini tamaa ikamuingia na kupata msukumo wa kutaka kushinda Zaidi.

Hapo ndipo alianza na kuweka kima cha Naira elfu 40 ambazo zilienda na kabla hajagutuka, akapata laki mbili zote zimeshakunywa maji ndani ya muda mfupi tu, na furaha ikageuka kuwa majonzi.

Video iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii ilinasa wakati wa kuhuzunisha kijana alijikuta kutokana na uwekezaji wake duni, na alionekana amejilaza kwenye godoro akiwa ameishiwa na nguvu huku akiwa hataki kabisa kuiona simu yake baada ya kupoteza mpunga.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya watu katika chapisho hilo;

benbills007 alisema: "Hilo ni jambo moja kuhusu kamari ๐Ÿ˜‚..Utashinda, lakini siku watakapoenda kukusanya pesa zako zote, utalia siku hiyo ๐Ÿ˜‚."

 

dansky_exchange alitoa maoni: โ€œDau kamwe si njia ya kupata pesaโ€ฆnyumba hakika itashindaโ€ฆUTPOTEZA PESA YAKO.:

 

mcjblazedwfc alitoa maoni yake: "Tukikimbia Pesa sasa atakwenda bado kubeba Man U kushinda au sare ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚."

 

king_cozzy_ alibainisha: "Pesa atatumia kununua shuka mpya ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚."