"Siwa'miss, siwafahamu!" Akothee afunguka kuhusu uhusiano mbaya na ndugu zake

"Siwamiss hata mmoja wao. Sisi ni ndugu kwa damu, lakini uhusiano na urafiki haupo tena," Akothee alisema.

Muhtasari

•Mwimbaji huyo aliyegeuka kuwa mjasiriamali alifunguka jinsi maisha yamekuwa tangu kukata mawasiliano yoyote na ndugu zake.

•Mama huyo wa watoto watano amewasamehe ndugu zake na kuweka mipaka.

Akothee
Akothee
Image: HISANI

Uhusiano mbaya kati ya Akothee na ndugu zake unazidi kuwa wazi.

Hawasalimiani tena, kulingana na kukiri kwake hivi majuzi mtandaoni.

Mwimbaji huyo aliyegeuka kuwa mjasiriamali alifunguka jinsi maisha yamekuwa tangu kukata mawasiliano yoyote na ndugu zake.

Mtumbuizaji huyo na dadake Cebbie Koks ndio maarufu zaidi mtandaoni na wawili hao hawazungumzi tena.

Akothee kwenye video ya Jumatano, Jan 24 usiku, alitangaza kwamba hatawa’miss tena.

"Chochote nilichoona na familia yangu mwaka wa 2022 kuelekea Desemba nisingependa mtu yeyote apitie hilo," alisimulia.

Alikuwa akimaanisha hali yake ya akili alipokuwa kwenye uhusiano ambao uliisha.

"Nilikuwa katika mazingira magumu nilijihisi peke yangu. Hiyo ndiyo hisia mbaya zaidi katika ulimwengu huu uliojaa watu. Hiyo ndiyo hisia mbaya zaidi ambayo mwanadamu yeyote anapaswa kuwa nayo. Hasa baada ya kusaidia karibu kila mtu. Inaumiza. Na kwa njia, naweza kusema. wewe wa mwili sana, nilikuwa na kizuizi kikubwa kati yangu na ndugu zangu."

Aliongeza;

"Siwa’miss kwa sababu si’miss shida"

Pia alisema haikuwa wazi ni nani kati yao alikuwa sumu

"Labda mimi ndiye niliyekuwa sumu, ni sawa. Unapokuwa sumu unachora mpaka basi hakuna ...umenielewa" Alitumia mikono yake kuashiria vuta nikuvute.

"Siwamiss hata mmoja wao, siwafahamu, sawa tukikutana kwa mzazi wangu, tuko na baba na mama mmoja. Sisi ni ndugu kwa damu, lakini uhusiano na urafiki haupo tena. Wewe ni vibe tu na watu ambao wanavibe na wewe," aliendelea kushiriki.

Mama huyo wa watoto watano amewasamehe ndugu zake na kuweka mipaka

"Nilimsamehe kila mtu lakini....*akitumia mkono wake kuchora mstari* kwa heshima. Sisi sio marafiki, We dont vibe. Vibe imeisha kwa sababu naogopa kuumizwa tena"

Hawasalimiani hata hadharani ili kujilinda

"Kwanini inatubidi? Nikiwasalimia nitaingia tena kwenye mtego, hata nitakutana nao hadharani na kuwapita. Nilichopitia hakikuwa na thamani, kilikuwa kikubwa sana."

Sasa ana amani na hana wasiwasi.

"Nilichopitia walinitawanya nikawa uchi, wakanirusha kwenye mitandao ya kijamii kwa uongo, unategemea nitavibe vipi na watu kama hao? Tunagawana damu, dhamana, tunashirikiana mama na baba lakini sio marafiki. ni sawa,".

Utafsiri: Samuel Maina