Mrembo amtaka mume mtarajiwa kuoa wake 4, "siwezi ishi kwa ndoa peke yangu" (Video)

Akiunga mkono hoja yake, mwanamke huyo alisema mume wake hawezi kuwa kwa ajili yake tu kwa sababu idadi ya wanawake ni zaidi ya wanaume katika jamii.

Muhtasari

• Kulingana na mwanadada huyo, yeye ni mtu anayejali kumaanisha kuwa mume wake hawezi kuoa tu na kuongeza kuwa hajali kuwa mke wa pili, wa tatu au wa 4.

Image: screengrab

Ingawa wanawake wengi wa hawaungi mkono ndoa ya wake wengi, video mpya ya mwanamke wa umri wa makamo akijihusisha na mitala imezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii.

Katika klipu hiyo mpya inayoenea mtandaoni, mwanadada huyo wa Nigeria aliyetambulika kwa jina la Tinuke Vibes kwenye Instagram alisema kuwa mume wake hawezi kumuoa peke yake.

Akituma ujumbe kwa mume wake mtarajiwa, mwanamke huyo anadai kwamba ikiwa mume wake hawezi kuoa wake wanne hawezi kamwe kumuoa.

Kulingana na mwanadada huyo, yeye ni mtu anayejali kumaanisha kuwa mume wake hawezi kuoa tu na kuongeza kuwa hajali kuwa mke wa pili, wa tatu au wa 4.

Akiunga mkono hoja yake, mwanamke huyo alisema mume wake hawezi kuwa kwa ajili yake tu kwa sababu idadi ya wanawake ni zaidi ya wanaume katika jamii.

Aliongeza kuwa kutokana na hili hawezi kuwa mbinafsi kiasi kwamba hataweza kumshirikisha mwanaume wake na wanawake wengine.

Akitoa ushauri kwa wanawake wa siku hizi, Atinuke aliwataka kubadili fikra zao ili amani itawale linapokuja suala la ndoa akiwataka kila wakati kuruhusu wanaume wao kuoa wake wengine.

Alihitimisha kuwa wanawake wanapaswa kufuata njia yake na pia kuolewa na mwanamume tajiri na mwenye uwezo.

 

Tazama video hapa chini;