'Mwanaume akiku'cheat, usimuache bali m'cheat pia' - Muigizaji wa kike ashauri kina dada (video)

Akitoa taarifa kulingana na uzoefu wake, Laide Bakare ambaye ana watoto watatu kutoka kwa zake mbili za awali anathibitisha kuwa wanaume wote huchepuka.

Muhtasari

• Kwa hiyo mhojiwa alimuuliza Laide Bakare “Kwa hiyo mwanaume akikusaliti kimapenzi utamsaliti tena?

• Akijibu, muigizaji alisema; "Nitachepuka."

Muigizaji Laide Bakare.
Muigizaji Laide Bakare.
Image: Instagram

Mwigizaji maarufu wa Nollywood Laide Bakare amezua hisia miongoni mwa watumiaji wa mtandao kufuatia madai yake ya hivi majuzi kuhusu wanaume wanaochepuka katika ndoa zao.

Laide Bakare ambaye alizua uvumi wa ndoa ya 3 wiki zilizopita anawaambia wanawake kwamba ikiwa wanaume wao watawasaliti kimapenzi, wanapaswa kuwasaliti pia, na si kuwaacha au kuvunja mahusiano.

Akiongea zaidi, Laide Bakare alifichua kuwa badala ya mwanamke kuvunja ndoa yake kwa sababu ya mwanamume kutokuwa mwaminifu, anapaswa kusalia kwenye ndoa na kumchepukia mumewe na mwingine.

Akitoa taarifa kulingana na uzoefu wake, Laide Bakare ambaye ana watoto watatu kutoka kwa zake mbili za awali anathibitisha kuwa wanaume wote huchepuka.

Laide Bakare zaidi anawaambia wanawake kufanya hivyo kwa viwango vyote vya ukomavu wanapojaribu kuwachepukia wanaume wao.

Kwa maneno yake; "Wanaume wote wanachepuka, wakati anachepuka ningesema usiondoke lakini unaweza kuchepuka, lakini lazima ufanye kwa viwango vyote vya ukomavu."

Kwa hiyo mhojiwa alimuuliza Laide Bakare “Kwa hiyo mwanaume akikusaliti kimapenzi utamsaliti tena?

Akijibu, muigizaji alisema; "Nitachepuka."

Tazama video hapa chini;