Justina Syokau afichua kuwa hajashiriki tendo la ndoa kwa takriban miaka 10

Amefichua mambo ya kushtua kuhusu maisha yake, akidai kuwa hajawa na uhusiano wa kimapenzi kwa takriban miaka 10.

Muhtasari

•Syokau alitaja kwamba anaogopa kuvuma kwenye mtandao wa Twitter ikiwa mwanamume aliyejihusisha naye kimapenzi atarekodi video ya kipindi chao cha pamoja.

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Image: HISANI

Mwimbaji wa nyimbo za injili  aliyezingirwa na utata mwingi Justina Syokau amefichua mambo ya kushtua kuhusu maisha yake na wanaume, akidai kuwa hajawa na uhusiano wa kimapenzi kwa takriban miaka 10.

Katika mahojiano ya hivi majuzi, Syokau alitaja kwamba anaogopa kuvuma kwenye mtandao wa Twitter ikiwa mwanamume aliyejihusisha naye kimapenzi atarekodi video ya kipindi chao cha pamoja.

"Naogopa kurekodiwa kwenye video, skuizi kuna kurekodi video, imagine mrembo hii yote ikionyeshwa wakenya, watu wakikutana Twitter juu ya ko....

kama ni jinsi nilivyoiacha miaka 10 iliyopita, unakuta ni tamu ambayo huwezi ku- kuratibu kamera ilipo," Justina alisema.

Miezi kadhaa iliyopita, mwimbaji huyo wa nyimbo za injili alizamia kwenye mitandao ya kijamii kueleza sifa anazotamani kwa mwanamume kutumia bango, jambo ambalo lilipuuzwa na baadhi ya mashabiki wake wakidai kuwa anatafuta umaarufu.

Mapema mwaka jana, Justina alifichua katika mahojiano na Mungai Eve kuwa sababu iliyomfanya kutochumbiana na mtu yeyote kwa miaka 10 iliyopita ni kwamba alipokutana nao mwanzoni walivutiwa naye hadi walipogundua kuwa ana mtoto kwani waliona mtoto. kama mzigo.