Zari avunja kimya kuhusu Diamond kuvunja ndoa yake na Shakib

Zari amejibu kuhusu kurudiana na mzazi mwenzake Diamond Platnumz.

Muhtasari

•Zari amejibu madai kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake akidokeza kuwa Diamond si sababu ya migogoro ya ndoa yake.

•Zari aliweka wazi kuwa uhusiano wake na Diamond haujafufuliwa na kuwataka watu kuacha kuzingatia masuala yao.

ZARI HASSAN
ZARI HASSAN
Image: INSTAGRAM

Ijumaa jioni, mwanasosholaiti maarufu wa Uganda Zari Hassan alijibu baadhi ya maswali na madai ambayo mashabiki wameibua kuhusiana na kile kinachoendelea kati ya uhusiano wake na ule wa mzazi mwenzake Diamond Platnumz.

Uvumi mwingi umeibuka ndani ya saa kadhaa zilizopita baada ya kuibuka kwa video inayomuonyesha mama huyo wa watoto watano akiwa ameshikana mikono kimapenzi na Diamond.

Miongoni mwa madai ambayo yameibuka ni kwamba ndoa ya Zari na Shakib imetiwa doa na kuvunjika baada ya video hiyo yenye utata kuibuka kwenye mitandao ya kijamii, madai ambayo sosholaiti huyo mrembo amejibu na kudokeza kuwa mzazi mwenzake huyo si sababu ya migogoro ya ndoa yake.

Shabiki mmoja alisema, “Zarinah wewe ni mrembo sana. Tafadhali usiruhusu Diamond kuharibu kitu kizuri ambacho wewe na Shakib mmejenga."

Alijibu, "Hana uhusiano wowote na 'sisi'

Huku akimjibu shabiki aliyemshauri dhidi ya kurudiana na baba wa watoto wake wawili wadogo, Zari aliweka wazi kuwa uhusiano wao uliovunjika miaka kadhaa iliyopita haujafufuliwa na kuwataka watu kutozingatia masuala yao.

"Nadhani nyote mna maoni ambayo hayana msingi. Nani kakwambia nimerudi naye au narudiana naye? Nyote pumzikeni, mna mengi yanayoendelea katika maisha yenu kuliko kuangazia yale ambayo si yenu,” sosholaiti huyo alisema.

Zari pia alikanusha madai ya kuvunja uhusiano wa Diamond na Zuchu akisema, "Kwani promotion ya nyimbo inaingiliaje kwa mapenzi, kwani kaka ashoot na wanawake wengine, nitolee upuuzi."

Kumekuwa na madai kuwa mume wa mwanasosholaiti huyo, Shakib Cham Lutaaya aligura ndoa yao baada ya kuonekana akitembea na Diamond.

Kwa upande mwingine, Zuchu alitangaza kuachana na Diamond Platnumz Ijumaa jioni, saa chache baada ya bosi huyo wa WCB kuonekana akiwa na Zari.#