Mrembo akiri kutumia dumba kupata mume tajiri, aonyesha maisha kabla na baada ya ndoa (video)

Kabla ya kutumia dumba, mrembo huyo alikuwa ni mfano hai wa tabu na shida asiyekauka machozi machoni, lakini miezi 3 tu baada ya kutumia dumba, alimpata mume tajiri.

Muhtasari

• Pia alipakia picha wakiwa wameketi ndani ya gari na mume huyo wakiwa wameshikana mikono kwenye gari la kifahari.

• Alianza kwa kuonyesha jinsi maisha yake kabla ya kutumia dumba na kumpata mume huyo yalivyokuwa ya mateso.

Image: Screengrab

Msichana mmoja kwenye mtandao wa TikTok amewashangaza watu baada ya kukiri kwamba alitumia dumba ili kuipata ndoa yake ya sasa.

Mrembo huyo anayekwenda kwa jina Mumzy Morgan alipakia video akionyesha jinsi maisha yake yalivyobadilika miezi mitatu tu baada ya kutumia dumba na kumpata mwanamume wake tajiri.

Alianza kwa kuonyesha jinsi maisha yake kabla ya kutumia dumba na kumpata mume huyo yalivyokuwa ya mateso.

Kabla ya kutumia dumba, mrembo huyo alikuwa ni mfano hai wa tabu na shida asiyekauka machozi machoni, lakini miezi 3 tu baada ya kutumia dumba, alimpata mume tajiri ambaye alikuwa anamgea burunguti na hela pamoja na zawadi zingine za kimalkia.

Pia alipakia picha wakiwa wameketi ndani ya gari na mume huyo wakiwa wameshikana mikono kwenye gari la kifahari.

Hata hivyo, katika upande wa kutoa maoni baadhi ya watumizi wa TikTok, wengi wao wakiwa wa kike walionekana kumtaka kuwaunganisha na mtoa dumba hiyo kwani walikuwa wamechoka na maisha ya kuungaunga kwenye uhusiano wao usio na tija.

“Tafadhali, dumba hiyo ni pesa ngapi,” Mummy First Lady aliuliza.

“Tafadhali hiyo dumba ni ya aina gani, ninaitaka pia,” Mma aliuliza pia.

“Mama nahitaji hirizi pia 😩🤲unaishi wapi?” Maryam.

“Mimi nitafutiwe mwanamume kwanza kabla ya kuanza kuzungumzia mambo ya dumba,” Ezther alisema.

Tazama video hiyo hapa chini;