Mke agundua rafiki yake wa karibu amekuwa akitumia juju kumpokonya mumewe (video)

Aliwashauri wapenzi kujikita katika maombi ili kupata ufunuo wa marafiki wa karibu nao kwani pengine hao ndio wanaoleta pepo la kukosana katika mahusiano bila kujua,.

Muhtasari

• Mrembo huyo alisema kwamba katika mahusiano mengi, kila mara wapenzi wanavurugana bila kujua kwamba marafiki zao wa karibu ndio wako nyumba ya kukorofishana huko.

Mrembo amtuhumu rafiki yake kwa kutumia juju kumpokonya mume
Mrembo amtuhumu rafiki yake kwa kutumia juju kumpokonya mume
Image: TikTok

Hivi, ni kweli kwamba kuna ushirikina ambao mtu anaweza akatumia ili kumpata mpenzi au kumpokonya mwenzake mwenzi wake?

Mwanamke mmoja katika mtandao wa TikTok amezua gumzo hilo baada ya kufanya video akiimtuhumu rafiki yake wa karibu kwa kutumia dumba kumchukulia mume wake.

Kwa mujibu wa mrembo huyo kwa jina Peace873, alisema kwamba rafiki yake wa kike kwa muda mrefu amekuwa na ukaribu usio wa kawaida kwa familia yake na haswa kwa mume wake.

Baada ya kumdadisi kwa kina, alikuja kugundua kwamba rafiki huyo wake alikuwa akimtaka mumewe kimapenzi lakini akashindwa.

Peace alidai kwamba baada ya rafiki yake kushindwa kumshawishi mumewe kumpenda yeye, aliamua kwenda kwa waganga wa jadi kwa ajili ya juju ili kumpokonya mume wake.

Kulingana na mke huyo, rafikiye Amaka amekuwa akijaribu kumpokonya mumewe na amefikia hatua ya kwenda ufukweni kulipa watu wa kumfanyia kazi za ulozi.

Alibainisha kuwa anamwanika hadharani kwa sababu hamuogopi tena.

“Huyu mrembo mnayemuona hapa amekuwa akijaribu kuchukua mume wangu. Nimeolewa ila sijawahi kuambia mtu yeyote, sipendi kuweka mambo yangu hadharani. Huyu amekwenda mbali Zaidi katika hatua za kukesha ufukweni kuwalipa watu pesa ili kumfanyia mambo ya ajabu. Kumpa dumba ili kunitenganisha na mume wangu. Amekuwa akifanya hivyo kwa njia mbali mbali. Hii ninaiweka hadharani mitandaoni Amaka kwa sababu sikuogopi,” alisema.

Mrembo huyo alisema kwamba katika mahusiano mengi, kila mara wapenzi wanavurugana bila kujua kwamba marafiki zao wa karibu ndio wako nyumba ya kukorofishana huko.

Aliwashauri wapenzi kujikita katika maombi ili kupata ufunuo wa marafiki wa karibu nao kwani pengine hao ndio wanaoleta pepo la kukosana katika mahusiano bila kujua,.