Wanafunzi wasichana wafanyishwa usafi hotelini baada ya kula na kushindwa kulipia (video)

"Mliambiwa muende nyumbani, nyinyi mkarukia kwa hoteli kula, halafu baada ya hapa mtaenda kuosha vyombo, harakisheni hamna muda wa kuharibu,” mhudumu wa hoteli aliwaambia.

Muhtasari

• Walimaliza kula chakula cha kifahari na walipoletewa bili, walidai hawakuwa na pesa.

• Waliamriwa kusafisha hoteli na kufanya kazi nyingine huku wakingoja wazazi wao watoe bili.

Wanafunzi wafanyishwa kazi kisa kushindwa kulipia chakula
Wanafunzi wafanyishwa kazi kisa kushindwa kulipia chakula
Image: Screengrab

Wasichana wa shule ya upili wenye ujanja walilazimika kutekeleza usafi katika mgahawa mmoja baada ya kula na kushindwa kulipia bili ya chakula.

Katika video ambayo imekuwa ikienezwa katika mtandao wa X, wasichana hao watatu waliokuwa wamevalia sare wanasemekana kuingia katika hoteli hiyo, kuitisha chakula lakini baada ya kula, walishindwa kulipia bili.

Walimaliza kula chakula cha kifahari na walipoletewa bili, walidai hawakuwa na pesa.

Waliamriwa kusafisha hoteli na kufanya kazi nyingine huku wakingoja wazazi wao watoe bili.

Kwenye video hiyo, mhudumu wa hoteli hiyo alionekana akiwapa vifaa vya kufanya usafi na kuwataka kutakatisha kila eneo hadi pale atakaporidhika kwamba kazi ambayo wamefanya inatosha kulipia bili ya vyakula walivyokula.

“Nyinyi, osha hapo, mnakula hamtaki kulipa. Mnadhani mmetoka shule sasa kazi yenu ni kutoka shule bila kulipa. Panga hapo vizuri, leo hamtaenda kokote, mtakaa hapa hadi pale wazazi wenu watakapowakujia.”

“Nyinyi wasichana mnashangaza sana, mnafikiria kisa mko shuleni mtaleta uchizi wenu hapa. Sasa nyinyi ndio hawa hapa, mliambiwa muende nyumbani, nyinyi mkarukia kwa hoteli kula, halafu baada ya hapa mtaenda kuosha vyombo, harakisheni hamna muda wa kuharibu,” mhudumu wa hoteli hiyo alisikika akiwaambia.

Kabla ya kumaliza, aliita mmoja wao kumpa namba ya simu ya mzazi ili akawataarifu mahali walipo na walichokifanya.

Tazama video hiyo hapa chini;