Mtangazaji wa kike aeleza sababu za kuacha kumkumbatia babake (video)

"Tukiwa wadogo tulikuwa tukienda chumbani kwa baba kucheza na kumkumbatia, asubuhi moja alinikumbatia na nikahisi msisimko wa uume wake, niligundua wakati wa kucheza na baba umekwisha."

Muhtasari

• Siku moja ambayo ilikuwa ya mwisho yeye kukumbatiana na babake, alimkumbatia na kuhisi uume wa mzazi wake ukisisimka.

• "Niligundua wakati huo kwamba wakati wa kucheza umekwisha. Sikuhitaji kufundishwa kuhusu hilo.” alisema.

Mtangazaji ahadithia kuhisi msisimko wa uume wa babake
Mtangazaji ahadithia kuhisi msisimko wa uume wa babake
Image: Instagram

Mtangazaji na mwigizaji wa kike maarufu nchini Nigeria kwa jina Katherine Obiang amezua gumzo pevu katka mitandao ya kijamii baada ya video kuibuka akihadithia jinsi alibadili mazoea ya kukumbatiana na babake.

Mrembo huyo alikuwa akizungumza kwenye kipindi kimoja cha runinga ambapo alimuona mwanamume mmoja akicheza densi ya bintiye wakikumbatiana.

Akizungumzia video hilo, Obiang aliikashifu na kuibua suala kuhusu kile kitakachotokea ikiwa baba atapatwa na msisimko wakati anakumbatiana na bintiye, ikizingatiwa kwamba ni jambo la kawaida kwa mwanamume kusisimka pindi anapokumbatiana na mwanamke.

Hili lilimfanya Obiang kukumbuka tukio moja akiwa na umri wa balehe ambapo kila asubuhi alikuwa anapenda kumkumbatia babake kwa salamu.

Siku moja ambayo ilikuwa ya mwisho yeye kukumbatiana na babake, alimkumbatia na kuhisi uume wa mzazi wake ukisisimka.

Alisema, “Tuseme alipokuwa akicheza dansi na bintiye namna hiyo na kusimika, nini kingetokea? Kwa sababu ni kawaida, yeye ni mwanaume.”

“Wakati tukiwa wadogo tulikuwa tukienda chumbani kwa baba kucheza lakini asubuhi unapotaka kumkumbatia baba yako kwa sababu unapenda anavyonusa, nilihisi msisimko wake na nikajipanga na hiyo ilikuwa mara ya mwisho kwa sababu nilijipanga. Niligundua wakati huo kwamba wakati wa kucheza umekwisha. Sikuhitaji kufundishwa kuhusu hilo.”

Tazama video hiyo akisimulia hapa chini;