Manzi wa Kibera athibitisha kifo cha ex wake wa miaka 67

Mzee huyo aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 67 siku ya Jumapili, Aprili 21.

Muhtasari

•Kifo hicho kilithibitishwa na Manzi wa Kibera ambaye alielezea kusikitishwa kwake na kifo cha ghafla cha mpenzi wake wa zamani.

Manzi wa Kibera na mpenzi wake wa zamani.
Manzi wa Kibera na mpenzi wake wa zamani.
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti Manzi wa Kibera amefiwa na aliyekuwa mpenzi wake, Peter Nzioki.

Mzee huyo aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 67 siku ya Jumapili, Aprili 21.

Kifo chake kinakuja miezi michache tu baada ya mwasosholaiti huyo kuonyesha mpenzi wake mpya, ambaye pia ni mzee kwenye mitandao ya kijamii.

Kabla ya kifo chake, Peter Nzioki na Manzi Wa Kibera walikuwa wameachana.

Mzee huyo alikuwa amemsihi yule mrembo huyo amrudie bila mafanikio.

Kifo hicho kilithibitishwa na mwanasosholaiti huyo ambaye alielezea kusikitishwa kwake na kifo cha ghafla cha mpenzi wake wa zamani.

Alifichua kuwa familia yake, ambayo ni pamoja na watoto watatu inasimamia maandalizi ya mazishi yake.

"Wale ambao hawaamini habari hizi, waende katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City na kumuona. Yupo na nimehuzunika sana. Familia yake inashughulikia kila kitu," alifichua.

Picha ya mwisho ambayo Manzi wa Kibera na mpenziwe huyo wa zamani walichapisha hadharani ilikuwa Desemba 30, 2023, walipoonekana wenye furaha sana.

Alikuwa ametumia Krismasi na Mzae, akitangaza kwa furaha upendo wao ni wa milele.

"Mapenzi anaishi hapa ❤️😍💋"

Manzi kisha siku moja baadaye alishiriki picha ya mpenzi wake wa zamani na mpya, akiikejeli kwa mzaha.

"Sasa yako ni ex wa mtu 🤣😂😁" aliandika.